Kufuatia kifo cha mke wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, alituma ujumbe wa rambirambi kwa Marja’ huyu mkubwa.
Ndoa ni heshima, ndoa ni stara ya kijamii, na ndio maana Qur'an Tukufu ikasema: «هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ» kwamba "Mwanamke ni vazi kwa Mwanaume, na Mwanaume ni vazi kwa Mwanamke". Katika kazi za vazi (nguo) ni heshima, kupendeza, kuheshimika, vazi kawaida yake linaleta heshima katika jamii, na Ndoa vile vile inaleta heshima katika Jamii.
Mume na Mke wako huru kutekeleza majukumu yao ya Faradhi ya Shariah, na kitendo cha wote wawili kiko chini ya idhini ya mwingine. Na funga (Saumu) ya Wajibu pia iko hivyo.