9 Mei 2025 - 01:21
Sheikh Dkt. Abdul- Razak Amiri Atoa Kisa Halisi Cha Mwanamke wa Kiislamu aliyedai Talaka kisa Mume Wake Kaoa Mke wa 2, Hatimaye naye akawa Mke wa Pili

Ndoa ni heshima, ndoa ni stara ya kijamii, na ndio maana Qur'an Tukufu ikasema: «هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ» kwamba "Mwanamke ni vazi kwa Mwanaume, na Mwanaume ni vazi kwa Mwanamke". Katika kazi za vazi (nguo) ni heshima, kupendeza, kuheshimika, vazi kawaida yake linaleta heshima katika jamii, na Ndoa vile vile inaleta heshima katika Jamii.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sheikh Dkt. Abdur-Razak Amiri, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), ametoa Kisa cha mmoja wa kina mama wa Kiislamu katika moja ya miji yetu ya Pwani ya Afrika Mashariki. Amesema: "Mama huyu alikuwa ni mke wa mtu. Lakini yule mumewe baada ya miaka kadhaa, akaamua kuoa mke wa pili. Baada ya mama yule (Mke wake wa kwanza) kugundua aliomba Talaka kwa mumewe.Kila ambavyo mume alijitahidi kujizuia kutoa Talaka, mama yule hakukubali. Hatima yake mume wake alilazimika kuitoa ile Talaka. Mama yule alipoachika, akarudi nyumbani, na akaishi na wazazi wake. Lakini yale maisha ya nyumbani baada ya kuachika, yalimfanya afikirie kuwa na mume. Na hatimae akapata mwanaume wa kumuoa, na akaolewa akiwa ni mke wa pili kwa mwanaume wa pili.

Sheikh Dkt. Abdul- Razak Amiri Atoa Kisa Halisi Cha Mwanamke wa Kiislamu aliyedai Talaka kisa Mume Wake Kaoa Mke wa 2, Hatimaye naye akawa Mke wa Pili

Tunajifuza nini kutokana na kisa hiki cha kweli?

Katika kisa hiki tunajifunza yafuatayo:

1-Mwanamke asirahisishe Talaka.

2-Na asidhani anaporudi nyumbani, thamani yake kwa wazazi itakuwa ni sawa sawa na thamani yake kabla hajaolewa.

3-Unapoolewa na Mwanaume, na unapoamua kuachika, haina maana ni kuwa na mwanaume na kuwa mbali na mwanaume, bali ina maana ya kuwa na heshima na kuepuka heshima.

4-Ndoa ni heshima, ndoa ni stara ya kijamii, na ndio maana Qur'an Tukufu ikasema: «هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ» kwamba "Mwanamke ni vazi kwa Mwanaume, na Mwanaume ni vazi kwa Mwanamke". Katika kazi za vazi (nguo) ni heshima, kupendeza, kuheshimika, vazi kawaida yake linaleta heshima katika jamii, na Ndoa vile vile inaleta heshima katika Jamii.

5-Hali kadhalika kwa Mwanaume, asirahisishe talaka. Mapema sana utakapomuacha mkeo, ile nyumba utaiona namna ambavyo imebadilika.Itakuwa ni nyumba ambayo haipendezi, ina huzuni, ina masononeko, na haina furaha. Utajua thamani ya mke baada ya kumuacha. Sasa jifunze kwa wenzako, na usiwe ni mtu ambaye wenzako watajifunza kwako wewe. Kwa hali kama hiyo, Uislamu umetia uzito katika Talaka, lakini umerahisisha sana katika Ndoa. Kwa sababu Mungu anatutaka tuingie kwa wingi katika Ndoa, lakini tusitoke kwa wingi katika Ndoa".

Wasslam Alaikum warahmatullah Taala wa Barakatuh

Sheikh Dkt. Abdur-Razak Amiri

08 - 05 - 2025

Sheikh Dkt. Abdul- Razak Amiri Atoa Kisa Halisi Cha Mwanamke wa Kiislamu aliyedai Talaka kisa Mume Wake Kaoa Mke wa 2, Hatimaye naye akawa Mke wa Pili

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha