ndoa
-
Kwa nini Ndoa ya Mitala isiyo Rasmi ("Ndoa Nyeupe" au White Marriage) ni tishio kwa Familia na Jamii?
Makala hii inachambua kwa mtazamo wa kina sababu za upinzani wa Uislamu dhidi ya ndoa nyeupe na inafafanua athari na madhara ya kijamii yanayosababishwa na aina hii ya ndoa.
-
Ndoa ya “Kiutendaji” na “Kimwitikio” katika Mtindo wa Maisha wa Kiislamu
Ndoa ya Kiutendaji (konshi) inajengwa juu ya msingi wa uelewa, upangaji, kuwa na malengo, na maarifa ya kina, ambayo yanaendana na mafundisho ya Qur'ani yanayosisitiza kutafakari na kutumia akili kwa kina. Kinyume chake, ndoa ya Kimwitikio (vakoneshi) hutokana na mashinikizo ya nje, pupa, na hisia za muda mfupi, hali ambayo inakinzana na mafunzo ya Qur'ani yanayohimiza kuepuka pupa na kufanya mashauriano. Kwa hivyo, uchaguzi wa ndoa wa kimakini na wa kuwajibika – yaani ndoa ya kiutendaji – unakubaliana zaidi na mtazamo wa Kiislamu.
-
Sheikh Dkt. Abdul- Razak Amiri Atoa Kisa Halisi Cha Mwanamke wa Kiislamu aliyedai Talaka kisa Mume Wake Kaoa Mke wa 2, Hatimaye naye akawa Mke wa Pili
Ndoa ni heshima, ndoa ni stara ya kijamii, na ndio maana Qur'an Tukufu ikasema: «هُنَّ لِبَاسٌ لَّكُمْ وَأَنتُمْ لِبَاسٌ لَّهُنَّ» kwamba "Mwanamke ni vazi kwa Mwanaume, na Mwanaume ni vazi kwa Mwanamke". Katika kazi za vazi (nguo) ni heshima, kupendeza, kuheshimika, vazi kawaida yake linaleta heshima katika jamii, na Ndoa vile vile inaleta heshima katika Jamii.
-
Kuangalia aina za "Istikhara" kwa mujibu wa Mtazamo wa Riwaya
Istikhara ni dhana (mafhumu) ya kidini ambayo ina (maana au) ufafanuzi wake na aina zake katika vyanzo vya kidini.