Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Kanuni ya Istikhara ni jambo linalokubalika, na hii ni kutokana na kwamba kuna hadithi nyingi juu yake; Kwa kadiri ambavyo Marehemu Shahidi wa Kwanza anasema kuhusu Hadithi hizi: “Hadithi hizi ni nyingi na ni mashuhuri miongoni mwa Masunni na Mashia”.[1]
Aina za Istikhara
Kuna aina kadhaa za istikhara katika elimu maarifa ya kidini:
1- Istikhara, kwa maana ya kuomba mema (kheri)
Aina hii ya istikhara ndiyo inayopendekezwa katika riwaya (hadithi) nyingi. Maana yake ni kumwomba Mwenyezi Mungu mema na ya kheri katika kila jambo.
Amirul-Mu’minin (amani iwe juu yake), alikuwa akiswali rakaa mbili, na baada ya hapo alikuwa akisema mara mia moja (100) “Astakhiru Allah / «أَستَخیرُ اللهَ» ” [Ninaomba kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu]; Kisha anasoma dua hii:
اللَّهُمَّ إِنِّي قَدْ هَمَمْتُ بِأَمْرٍ قَدْ عَلِمْتَهُ فَإِنْ کُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّهُ خَیْرٌ لِي فِي دِینِي وَدُنْیَايَ وَآخِرَتِي فَیَسِّرْهُ لِي، وَ إِنْ کُنْتَ تَعْلَمُ أَنَّهُ شَرٌّ لِي فِي دِینِي وَدُنْیَايَ وَآخِرَتِي فَاصْرِفْهُ عَنِّي کَرِهَتْ نَفْسِي ذَلِكَ أَمْ أَحَبَّتْ فَإِنَّکَ تَعْلَمُ وَلاَ أَعْلَمُ وَ أَنْتَ عَلاَّمُ الْغُیُوبِ.
Ee Mwenyezi Mungu! Hakika nilitilia maanani kufanya jambo ambalo Wewe unalijua. Ikiwa unajua kuwa jambo hilo ni kheri kwangu katika Dini yangu, Dunia yangu na Akhera yangu, basi nifanyie wepesi katika jambo hilo, na ikiwa unajua kuwa [jambo hili] ni shari kwangu katika Dini yangu, Dunia yangu na Akhera yangu, niondolee (na uniepushe na jambo hilo), sawa sawa nafsi yangu iwe ni yenye kuchukizwa na hilo au kufurahia (na kulipenda), hakika Wewe ndiye mwenye kujua na mimi sijui, na Wewe ni Mjuzi zaidi wa mambo ya siri (ghaibu). [2]
Muhaddithi mashuhuri, Sheikh Abbas Qomi, pia anasema katika Mafatih al-Jinan: Maana ya istikhara ni kuomba kheri; Kwa hivyo chochote unachotaka kufanya, muombe Mwenyezi kwa kheri yako.
Na imepokewa kwamba katika sijda (sajda) ya mwisho wa Sala ya usiku, omba kheri kwa Mwenyezi Mungu na useme mara mia moja (101):
“Astakhiru Allah Birahmatih / «أَستَخیرُ اللهَ بِرَحمتِه» ” [Ninaomba kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Rehma Zake];
2- Istikhara Kabla ya Kushauriana
Imam Sadiq (a.s), Kiongozi wa ukweli na uhakika, anasema: Wakati wowote unapotaka kufanya jambo (lolote), usishauriane na mtu yeyote mpaka ushauriane (umuombe) Mola wako.
Msimulizi akauliza: Je!, Nitamuombaje Mungu wangu?.
Hadhrat Imam Sadiq (a.s) akasema: Sema mara mia (100): “Astakhiru Allah / «أَستَخیرُ اللهَ » ” [Ninaomba Mwenyezi Mungu Kheri];" Kisha shauriana na watu ambapo Mwenyezi Mungu atamimina kheri yako kupitia ulimi wa yeyote yule ampendaye.[3]
3_ Istikhara ya Moyo
Mtume Muhammad (s.a.w.w) alimwambia mmoja wa Masahaba zake: Ewe Anas! Unapoamua kufanya jambo, omba kheri kwa Mola wako mara saba (7). Kisha angalia ni kitu gani cha kwanza kinachokuja moyoni mwako. Kheri ipo kwenye kile kitu (kilichokuja) kilichoangukia moyoni mwako; Yaani: Fanya hicho hicho.[4]
4- Istikhara kwa Njia ya Kawaida
Katika aina hii ya Istikhara, mtu hatosheki na Dua tu; Bali, anafanya kwa kitendo kinachobainisha wajibu wake (au kinachomung'amulia jambo lake); Kama vile kufanya Istikhara kwa Qur'an, kwa Tasbih, au Istikhara ya kutumia vipande vya karatasi.
Ama katika kuchagua Mwenzi wa ndoa (Mke), kwa hakika haiwezekani kabisa kwetu kuelewa kila kitu kilicho ndani ya mtu mwingine.
Katika suala la ndoa, hatua ya kwanza unayotakiwa kuichukua ni wewe kujijua kwanza unataka nini, na kuamua au kuainisha katika nafsi yako vigezo, sifa na matarajio uliyokuwa nayo au unayoyatarajia kuyaona kwa upande mwingine (kwa maana kwa huyo unayetaka kuingia naye katika ndoa). Utakapoona upande mwingine una sifa zote unazozipenda, lakini bado ukawa na shaka shaka hivi, basi unatakiwa kuendelea na suala lako hilo (usiache lakini) kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kulikabidhi au kuliweka suala lako kwenye njia ya Tawassuli.
Katika Istikhara kwa ajili ya kuoa (ndoa), sifa za ndani za mtu na zilizofichwa ndani yake, kwa hakika hazitambuliwi. Kwa hiyo, katika hili kinacho faa kwako kufanya ni hicho kwamba utakapoona upande mwingine (kwa huyo unayetarajia kumuoa au kuolewa naye) kuna sifa zote unazozipenda na kuzitaka, lakini bado ukawa na shaka shaka hivi, basi usiache endelea na jambo lako hilo (kwa maana, kama upange kuoa au kuolewa, usisite kufanya hivyo, lakini) kwa kutawakali kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t), na kulikabidhi au kuliweka jambo lako kwenye njia ya Tawassuli.
Istikhara kwa Kutumia vipande vya Karatasi
Istikhara hii ni katika aina ya istikhara ya kawaida ambapo utaifanya namna hii kama ifuatavyo:
Wakati wowote unapoamua kufanya jambo, tayarisha vipande sita (6) vya karatasi, andika kwenye karatasi tatu maneno haya: "بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمنِ الرَّحيمِ / Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu / خِيَرَةٌ مِنَ اللَّهِ الْعَزيزِ الْحَكيمِ لِفُلان بْنِ فُلان اِفْعَلْ / Kuomba kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, Mwenye Hekima, kwa ajili ya fulani bin fulani, Fanya."
Na katika karatasi zingine tatu andika neno hili:
" لا تَفعَلْ / Usifanye"
Kisha uziweke karatasi hizo sita chini ya mahala pako unakoswalia (yaani: Chini ya msala wako unaoutumia kuswali), na kisha uswali rakaa mbili kwa nia ya istikhara. Ukimaliza kuswali rakaa mbili na kutoa salam, kisha unasujudu, na ukiwa katika hali ya kusujudu unasema maneno haya mara mia moja (100):
“Astakhiru Allah Birahmatih Khiyaratun Fi A'fiyat / «أَستَخیرُ اللهَ بِرَحْمَتِهِ خِيَرَةً في عافِيَةٍ» ” [Ninaomba kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa Rehma Zake, Kheri katika afya].
Kisha unakaa chini (unatoka katika Sajda na Kukaa chini) na unasema maneno maneno haya:
اَللّهُمَّ خِرْ لي وَاخْتَرْ لي فىيجَميعِ اُمُوري في يُسْرٍ مِنْكَ وَعافِيَةٍ
"Eee Mwenyezi Mungu! nipe kheri, na unichagulie la kheri katika mambo yangu yote, katika raha (wepesi) na afya kutoka kwako"
Kisha unatoa karatasi zote sita chini ya mswala wako, kisha unazichanganya karatasi hizo pamoja (na kuziweka sehemu moja au kwenye chombo kimoja), kisha unaanza kutoa karatasi moja baada ya nyingine. Utakapoona karatasi tatu zilizoandikwa neno (اِفْعَلْ / Fanya ) zimetoka kwa kufuatana kwa mkupua mmoja, basi utafanya kile ulichotaka kukifanya, na ikiwa vikaratasi vitatu vilivyoandikwa neno "لا تَفعَلْ / Usifanye" havitatoka kwa kufuatana, na ikiwa karatasi moja itatoka iliyoandikwa (اِفْعَلْ / Fanya), na na nyingine ikatoka iliyoandikwa "لا تَفعَلْ / Usifanye", basi endelea kutoa hivyo hivyo mpaka zifike karatasi tano (5), na wakati huo uwe makini na uzingatie hili kwamba: Ikiwa karatasi hizo (5) ulizotoa, tatu kati yake zimeandikwa (اِفْعَلْ / Fanya) , na mbili zimeandikwa "لا تَفعَلْ / Usifanye", basi unaweza kufanya jambo lako ulilolikusudia kulifana, lakini ni kinyume chake, kwa maana ikiwa karatasi hizo (5) ulizotoa, tatu kati yake zimeandikwa "لا تَفعَلْ / Usifanye", na mbili zimeandikwa (اِفْعَلْ / Fanya) , basi hutakiwi kufanya jambo hilo.
Your Comment