Maneno haya ni wito wa kutuweka kwenye mstari wa Ucha Mungu, uwajibikaji wa nafsi, na kujiepusha na dhambi kwa kutambua kuwa hakuna kisichojulikana mbele ya Mwenyezi Mungu (swt).
Hadithi sahihi na iliyothibitishwa kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ni yenye lafdhi hii isemayo:
«وأهل بیتي» / "Na Ahlul-Bayt wangu”, ama riwaya ile ambayo imepachikwa lafdhi au neno «وسنّتي» / “Na Sunna yangu” badala ya lafdhi ya asili na sahihi isemayo: «وأهل بیتي» / "Na Ahlul-Bayt wangu”, riwaya hiyo ni batili kwa mtazamo wa sanadi ya upokezi wa Hadithi husika.