Ayatollah Sistani
-
Mwakilishi wa Ayatollah Sistani Ataongoza Swala ya Janaza ya Kiongozi Shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika Haram ya Imam Hussein (a.s)
Uongozi wa Ataba Tukufu ya Imam Hussein (a.s.) umetangaza kukamilisha maandalizi yote ya kupokea msafara wa mazishi ya Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, huku swala ya janaza ikitarajiwa kuongozwa na mwakilishi wa Marjaa Mkuu Ayatullah Sayyid Ali al-Sistani, Sheikh Abdul Mahdi al-Karbala'i.
-
Ayatollah Sistani ametangaza kesho (Alhamisi) kuwa ni Siku ya Kwanza ya Ramadhani
Ali al-Sistani ametangaza kuwa kesho Alhamisi ni siku ya Kwanza ya Ramadhani 1447H.
-
Jibu la Ayatollah Al-Udhma Sistani Kuhusu Kufuata Maimam wa Sala ya Jamaa Wanaopokea Malipo (Mishahara) za Kiserikali
Ayatollah Al-udhma Al-Sistani, kiongozi mkuu wa Shi’a, katika jibu lake kwa swali kuhusu kufuata maimamu wa sala ya jamaa (imam wa jamaa) wanaopokea haki (ya mishahara) kutoka serikali za Kiislamu, alishauri waumini wasisali nyuma yao, ili nafasi za kidini zilindwe dhidi ya uingiliaji wowote unaowezekana wa serikali.
-
Ujumbe wa Rambirambi wa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Ayatollah Sistani kufuatia Kifo cha Mke Wake
Kufuatia kifo cha mke wa Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Sistani, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, alituma ujumbe wa rambirambi kwa Marja’ huyu mkubwa.
-
Ayatollah Sistani Aitaka Dunia ya Kiislamu Kuchukua Hatua Haraka Kuhusu Njaa Inayoikumba Gaza
Kauli ya Ayatollah Sistani inakuja wakati ambapo mashirika ya misaada ya kibinadamu yanaonya kuwa njaa inasambaa kwa kasi kote Gaza, huku takwimu za Umoja wa Mataifa zikionesha kuwa karibu watu nusu milioni wanakumbwa na viwango vya juu vya njaa kali.