5 Aprili 2025 - 17:30
Majukumu ya Mwanalimu na Mwanafunzi (1)

Majukumu ya Mwalimu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu :- Majukumu yake binafsi, majukumu juu ya wanafunzi wake, na majukumu yake akiwa darasani.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) – ABNA – Makala hii inaongelea maudhui muhimu ya Kiakhlaq inayohusiana na adabu za mwenye kujifunza pamoja na adabu za mwenye kufundisha. Yapo majukumu ya Mwalimu na pia yapo majukumu ya Mwanafunzi. Mwalimu anatakiwa kuzingatia majukumu yake na kuyatimiza, na vile vile Mwanafunzi anatakiwa kutimiza majukumu yake. Katika sehemu hii, tutaishia katika kuangazia Majukumu ya Mwalimu na vigawanyo vyake vikuu vitatu. Na sehemu ijayo tutaangazia Majukumu ya Mwanafunzi na vigawanyo vyake vikuu vitatu.

Mwenyeezi Mungu (s.w.t) anasema ndani ya Qur’an Tukufu: “ Sema: Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua”. Rejea: Suratuz-Zumar (39), Aya ya 9.

Majukumu ya Mwalimu

Majukumu ya Mwanalimu na Mwanafunzi (1)

Majukumu ya Mwalimu yamegawanyika katika sehemu kuu tatu :- Majukumu yake binafsi, majukumu juu ya wanafunzi wake, na majukumu yake akiwa darasani.

  1. Majukumu yake binafsi .

       Ni jukumu la kila Mwalimu awe na sifa hizi.

  1.  Ikhlasi katika nia. Kazi yake ya kufundisha aifanye kwa ajili ya Mwenyeezi  Mungu (s.w), na pia yale anayoyasema yaendane na matendo yake. Ikiwa maneno yake hayaendani na matendo yake, basi hakika yatakosa uzito na hayatakuwa na athari yoyote kwa wanafunzi maana baadhi ya wanafunzi watasema: Kama maneno ya mwalimu ni ya kweli basi angeliyafanyia kazi kwanza ili awe mfano bora kwetu katika hayo ayasemayo.

Hata tukizifunua kurasa za Qur’an  Tukufu tutakutana na Maneno haya Matukufu ya Allah (s.w.t) akihoji:

“Je, mnawaamuru watu kutenda mema na mnajisahau wenyewe na hali mnasoma kitabu?. Basi hamfahamu”.Rejea:Suratul-Baqarah (2) : Aya ya  44.

Imam Jaafar Swadiq (a.s) aliulizwa kuhusu makusudio ya Aya hii Tukufu: “Kwa hakika wanao muogopa Mwenyeezi Mungu miongoni mwa waje wake ni wale tu wenye ujuzi”. Rejea : Surat Faatir (35): Aya ya 28.

Akasema Imam Jaafar Swadiq (a.s): Ni Yule ambaye tendo lake linaendana na kauli yake, na ambaye tendo lake haliendani na kauli yake huyo hana elimu”.

  1.     Ni juu ya kila Mwalimu kujipamba na tabia nzuri, kwani mwalimu anaathari kubwa katika jamii. Na mwenendo wake (tabia yake) unaathiri zaidi kuliko hata maneno yake.
  2.     Mwalimu asiwe bakhili katika kutoa elimu, aamrishe mema na akataze maovu.

Majukumu ya Mwanalimu na Mwanafunzi (1)

(ii)    Majukumu ya Mwalimu juu ya wanafunzi wake. Ni lazima kwa kila    Mwalimu kuwa na sifa hizi juu ya wanafunzi wake.

  1.     Awafundishe tabia njema, na maadili.
  2.    Mwalimu afanye juhudi kuwaeleza wanafunzi wake juu ya malengo ya    

   kutafuta elimu.

  1.    Mwalimu ajenge uhusiano wa kiudugu wa Kiislamu,yeye na wanafunzi wake.    

   Mwalimu awachukulie wanafunzi kama watoto wake. Na awapendelee mazuri   

   kama anavyo ipendelea nafsi yake.

          Amesema Mtume Muhammad (s.a.w.w):“Hata amini mmoja wenu mpaka  ampendelee ndugu yake kile anachokipenda katika nafsi yake”.

  1.    Mwalimu awatahadharishe wanafunzi wake juu ya maasi, na maovu.

          Na njia ya mwalimu iwe nzuri, kwa kutoa ushauri au nasaha au mawaidha au  

   maelekezo.

  1.    Mwalimu asiwe na tabia ya kujiona, kiburi na kujidai mbele ya wanafunzi

   wake na katika jamii kwa ujumla.

   Ni vizuri awe mpole, mcheshi, mwenye huruma na mwenye upendo.

  1.    Mwalimu awafundishe wanafunzi wake kujiamini kujitegemea katika nyanja     

   mbali mbali.

(iii)   Majukumu ya Mwalimu akiwa darasani.

           Ni juu ya kila mwalimu akiwa darasani awe na sifa hizi.

  1. Mwalimu afanye maandalizi mazuri kabla ya kuingia darasani, na maandalizi yasiwe upande wa masomo tu, bali maandalizi hata ya muonekano wake, usafi, umaridadi, utanashati, na utulivu wake.
  2. Mwalimu akiingia darasani asalimiane na wanafunzi wake, kwa kuwajulia hali zao. Akae sehemu ambayo wanafunzi wote watamuona.
  3. Mwalimu awe na muhtasari wa kufundisha atumie mbinu mbali mbali za kufundishia, pia afahamu uwezo wa wanafunzi wake.
  4. Mwalimu awe na kifua kipana, mvumilivu, asikilize maswali ya wanafunzi kwa uangalifu. Kwani baadhi ya maswali yana malengo mengine, inawezekana mwanafunzi anauliza swali kumpima mwalimu wake juu ya uvumilivu wake, hasira zake.

Inawezekana mmoja wao anakusudia kabisa kutumia maneno ya kuudhi. Ni juu ya mwalimu anapojibu maswali hayo, ajibu kwa utulivu, akitumia elimu yake zaidi, na ujuzi wake wa kiuwalimu.

Na Mwalimu akiulizwa jambo asilolijua, aseme sijui jambo hilo, na nipeni muda nikalichunguze, mwalimu yeyote atambue kuwa na sio aibu kusema sijui kama jambo hulijui.

(f)      Mwalimu kabla ya kumaliza somo lake, atilie mkazo katika nukta muhimu za

           somo hilo. Na awahamasishe wanafunzi wake juu ya tabia nzuri, kuwaheshimu   

           wengine na kujua majukumu yao katika jamii.   

           Hayo ni baadhi ya  majukumu. Tuangalie majukumu ya mwanafunzi kwa

           ufupi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha