Akisisitiza umuhimu wa kuunganisha maarifa ya Qur'an na matendo ya kijamii, Rais wa Iran amesema: Tatizo kubwa ni pengo kati ya kuijua na kuitekeleza Qur'an. Tunadai kuwa Qur’an inatuonyesha njia ya uongofu na inamfikisha Mwanadamu katika kilele cha juu zaidi, lakini ikiwa kivitendo hakuna dalili ya mwongozo huu inayoweza kuonekana katika maisha yetu ya kibinafsi na ya kijamii, basi kwa hakika tunapaswa kuangalia upya tabia zetu.
"Kila Muislamu anapaswa kuamini kuwa: Kuwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni fursa ya wakati. Hivi ndivyo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wa Mtume (a.s) pamoja na Masahaba wema walivyokuwa wakiamini, kwao Ramadhani haukuwa ni Mwezi kama Miezi mingine".