6 Aprili 2025 - 17:33
Majukumu ya Mwanafunzi yamegawanyika katika sehemu kuu tatu (2)

Amesema Mtume (s.a.w.w): “Mfano wa anaye jifunza akiwa mdogo ni kama Anaye nakishi (anaye chora) katika jiwe, na anaye jifunza ukubwani ni kama  na anayeandika katika maji”. Japokuwa kutafuta elimu ni vizuri na muhimu katika umri wote, lakini ukiwa katika umri mdogo ndio vizuri zaidi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul - Bayt (a.s) - ABNA - Katika makala iliyotangulia tuliashiria juu ya Majukumu ya Mwalimu na vigawanyo vyake. Katika sehemu hii ya pili tutazungumzia kwa ufupi juu ya Majukumu ya binafsi ya Mwanafunzi, majukumu ya Mwanafunzi juu ya Mwalimu wake, na majukumu ya Mwanafunzi akiwa Darasani.

  1.   Majukumu ya mwanafunzi binafsi.

(a)    Mwanafunzi afanye maandalizi ya kibinafsi katika kutafuta elimu, na pia umri mzuri wa kutafuta elimu ni wakati wa udogoni na ujanani.     

Amesema Mtume (s.a.w.w): “Mfano wa anaye jifunza akiwa mdogo ni kama Anaye nakishi (anaye chora) katika jiwe, na anaye jifunza ukubwani ni kama  na anayeandika katika maji”. Japokuwa kutafuta elimu ni vizuri na muhimu katika umri wote, lakini ukiwa katika umri mdogo ndio vizuri zaidi.

(b)    Ni juu ya mwanafunzi ajiepushe na kila kitu kinacho ushughulisha ubongo wake.

Kutafuta elimu kunahitaji subira, uvumilivu, kujitambua, na kujiepusha na matamanio.Na vile vile mwanafunzi ni lazima awe na malengo makubwa kuelekea mustakbali wake.

  1.   Majukumu ya wanafunzi juu ya mwalimu wao.
  2.   Kwanza ni lazima mwanafunzi achague mwalimu mwema, kwani mwalimu anayo nafasi kubwa sana katika kuwalea wanafunzi na kuwaongoza katika tabia iliyokuwa nzuri.
  3.   Wanafunzi washirikiane na mwalimu wao kama kwamba ni mzazi au zaidi ya mzazi wao.

Kwani wazazi sana sana wanawalea watoto wao katika upande wa kimwili, lakini mwalimu anawalea wanafunzi katika upande wa maadili na kiroho ambayo ni muhimu zaidi.

(c)   Mwanafunzi amheshimu mwalimu wake, na akimtaja mwalimu wake amtaje  kwa  heshima,na asisahau juhudi zake.

  1.  Majukumu ya wanafunzi darasani.

         Wanazuoni wa Akhlaq au Tabia wanawasisitiza wanafunzi kufanya au kuyatambua yafuatayo.

  1.  Mwanafunzi ajue uwezo wake wa kielimu, asije kujibebesha elimu asiyokuwa na uwezo nayo.
  2.  Mwanafunzi ategemee muhtasari uliosahihi katika elimu na maarifa.

         Mwanafunzi awe na ratiba ya kujisomea na aifuate vizuri kwa kila siku, atumie muda wake vizuri, kwani muda ndio rasilimali.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha