Hafla hiyo imetambuliwa na wadau wengi kama mfano bora wa jinsi maadhimisho ya kiroho yanavyoweza kujenga utulivu, upendo na mshikamano wa kijamii nchini Tanzania.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) imefanyika kwa utukufu mkubwa katika Masjid Majmuat Al-Islamiyyat - Temeke Mwisho, Jijini Dar es Salaam, Tanzania, mnamo tarehe 17 Oktoba 2025 (Ijumaa). Tukio hili lililopewa jina la “Maulid ya Mthamini wa Amani” limevutia viongozi wa dini, wanadiplomasia, na wageni wa kimataifa kutoka mataifa mbalimbali.
Hafla hiyo iliandaliwa na Masjid Majmuuat kwa uratibu wa Dr. Alhadi Musa Salum Al-Naqshbandiy ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Taifa (JMAT-TAIFA).
Miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria ni:
1_Balozi Mdogo wa Misri.
2_Aliyekuwa Mufti wa Kenya, Sheikh Omar Buya.
3_Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Dr.Abubakar Zubair bin Ally, aliyemuwakilishi Mgeni Rasmi wa Hafla, Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kasim Majaliwa.
4_Pamoja na viongozi mbalimbali wa dini za Uislamu, Ukristo, Ubuddha n.k, sambamba na wageni kutoka kabila la Waru nchini Korea.
Wakati wa maadhimisho hayo, tuzo maalum zilitolewa kwa viongozi wa dini waliotoa mchango mkubwa katika kukuza amani, udugu na maelewano ya kijamii, wakiwemo:
1_Mufti Mkuu wa Tanzania.
2_Sheikh Dr.Alhad Mussa Salum (Mwenyekiti JMAT-TAIFA).
3_Askofu Dr.Gabriel Maasa (Karibu Mkuu JMAT-TAIFA).
2_Mchungaji Mwamposa.
3_Prof. Habib Mazinge.
4_Shekh Walid Alhadi,
5_Sheikh Hemed Jalala, na wengine wengi.
Katika hotuba yake, Dr. Alhadi Musa Al-Naqshbandiy alisisitiza kuwa Maulidi si tu sherehe ya kidini, bali ni jukwaa la kukuza hekima, maadili, na umoja wa kitaifa.
Hafla hiyo imetambuliwa na wadau wengi kama mfano bora wa jinsi maadhimisho ya kiroho yanavyoweza kujenga utulivu, upendo na mshikamano wa kijamii nchini Tanzania.
Your Comment