Kupitia mihadhara hii, waumini hupata fursa ya kujifunza misingi ya itikadi, maadili ya Kiislamu, na mwongozo wa maisha unaojengwa juu ya haki, uadilifu na kumcha Mwenyezi Mungu.
Kibri ni ugonjwa wa moyo unaoharibu uhusiano wa mwanadamu na Allah, watu, na hata nafsi yake. Kwa mwanafunzi wa Hawza, kibri ni hatari zaidi kwani huua baraka ya elimu na huzuia nuru ya maarifa kuingia moyoni. Njia ya wokovu ni unyenyekevu (tawadhu’), kwani Mwenyezi Mungu huwanyanyua walio wanyenyekevu na kuwashusha wenye kibri.
Hadithi ya Mgawanyo wa Majukumu kati ya Imam Ali (a.s) na Bibi Fatima Zahra (s.a)
Hadithi inayosimulia jinsi Mtume Mtukufu (s.a.w.w) alivyogawa majukumu ya kifamilia kati ya Imam Ali (a.s) na Bibi Fatima (a.s) ni mfano wa hekima katika ujenzi wa familia ya Kiislamu.