10 Aprili 2025 - 14:43
Nukta 7 na Muhimu za Tabia Njema, Zilizosheheni Hekima na Busara

"Mwenyezi Mungu ameumba Viumbe Tofauti tofauti, na kila kimoja amekipa sifa zake , Ni Tatizo sana unapo taka  Sifa za Kuku awenazo Bata".

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA - Samahat Sheikh Rajab Sha'ban, Mtafiti na Mchambuzi wa masuala ya Kidini, amabainisha nukta saba za Kiakhlaq ya Kiislamu ambazo ni muhimu kwa kila Muislamu bali kila Mwanadamu kujipamba nazo. Uislamu umetufunza maadili na tabia njema.

Hapana shaka kwamba Tabia Njema ni sifa bora miongoni mwa sifa bora za Manabii wa Mwenyezi Mungu, pia ni sifa bora za Watu wale wanaosifika kwa sifa ya ukweli (Wakweli kama walivyotajwa ndani ya Qur'an) na watu Wema (miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu). Kupitia Tabia njema, Mwanadamu hupandishwa daraja ya juu kabisa, na hupandishwa cheo na Heshima Mbele za Mwenyezi Mungu. Na Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w) amefikia kilele cha juu jabisa cha Tabia njema kiasi kwamba mpaka Mwenyezi Mungu akathibitisha hilo ndani ya Qur'an Tukufu pindi alipomzungumzia Mtume Muhammad (s.a.w.w) akisema kwamba: "Hakika wewe uko Juu ya kiwango adhimu cha Tabia Njema".

Sisi kama wafuasi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), tuna kila sababu ya kuishi maisha ya kimaadili kama alivyoishi Mtume wetu Muhammad(s.a.w.w), na tumuige kwa kila kitu. Katika sehemu hii tutaashiria juu ya nukta saba na muhimu za kiakhlaq / tabia njema, na ni matarajio yetu kuwa nukta hizi atakayejipamba nazo atakuwa amezidi kujikurubisha zaidi kwa Mola wake Mtukufu, na hatimaye kuvuna heshima na daraja ya juu na kuwa pamoja na wakweli na watu wema, na hivi ndivyo alivyotuelekea Mwenyezi Mungu pale anaposema: "Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na kuweni pamoja na Wakweli". (Surah At-Tawba: Aya 119).

Nukta 7 na Muhimu za Tabia Njema, Zilizosheheni Hekima na Busara

Nukta hizo saba za kiakhlaq (Tabia njema), na zilizosheheni Hekima na Busara ni hizi zifuatazo:

1- Kusikia Mabaya yetu kila wakati haitusaidii, kuna Muda tunahitaji kusikia Mazuri yetu  ili tuache kufanya Mabaya.


2- Mwanaadam ana Kapu Mbili za kuhifadhi Matendo ya Watu, Kapu la Mazuri liko Nyuma yake, lakini Kapu la Mabaya liko Mbele yake, Hivyo Kuwa na Subra.


3- Kwenye Maisha Kuna Mengi Tunapitia, Ila kuna Mengine hatupaswi kuyasahau  ili yawe Funzo wakati Mwingine. 


4- Wazazi Ni Shina na Watoto ni Matawi, Basi unapofaidika na Matawi  Usisahau Kuthamini Shina pia.


5- Katika Maisha kuna Muda Unaishi na Rafiki za watu, na Rafiki zako wanaishi na watu wengine,  Kuna Muda Ukifika kila Mtu atakutana na Rafiki yake.


6-Katika Maisha kila Mwanaadam akijua nafasi yake kwa Mwingine, Basi  siku zote Amani Itatawala Sehemu husika.


7-Mwenyezi Mungu ameumba Viumbe Tofauti tofauti, na kila kimoja amekipa sifa zake , Ni Tatizo sana unapo taka  Sifa za Kuku awenazo Bata.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha