Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dkt. Masoud Pezeshkian, katika ujumbe wake kwa kongamano la kuheshimu wahifadhi na wahudumu wa Markazi ya Qur’ani Tukufu, amesema kuwa Aya za Qur’ani ni mwaliko wa kutafakari kwa undani, mwaliko unaoweza kuangazia na kuongoza maisha na mienendo ya mwanadamu.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya AhlulBayt (a.s) akieleza kuwa tabia njema ya Mtume (s.a.w.w) ilikuwa ndiyo sababu kuu ya ushawishi wake, aliongeza: "Popote palipo na maadili ya Mtume, hakika yataacha athari yake.