Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wanafunzi wa Chuo cha Masomo ya Dini – Hawzat al-Qaim (AJTFS) kilichoko chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Tanga wameanza Mtihani wa Robo ya Pili ya mwaka 2025 siku ya Ijumaa, tarehe 23 Mei 2025.
Mtihani huu ni sehemu ya ratiba ya kila mwaka ya Ki-Hawza inayojumuisha vipindi vinne vya mitihani (robo).
Mitihani hii inatarajiwa kukamilika Alhamisi ya wiki hii. Kitengo cha Ripoti za Hawza kinawatakia wanafunzi mafanikio mema na kuwaombea Tawfiq na ufaulu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Insha’Allah.
Your Comment