Kwa Mujibu wa Ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA -; Siku ya Quds Duniani kwa ajili ya kuungana na wadhulumiwa wa Palestina ilifanyika katika Mji wa Tanga - Tanzania, chini ya Usimamizi wa na Ushirikiano wa Taasisi ya mbili za Kiislamu: Taasisi ya Kiislamu ya Falah Islamic Foundation na Al_Furqan Foundation.
Limekuwa ni Kongamano Muhimu na lenye natija chanya katika Jamii ya Waislamu na Watu wa Tanga na viunga vyake, na mafanikio haya hakuna shaka kuwa yametoka na juhudi kubwa za Taasisi hizo na uratibu mzuri na maridhawa wa viongozi wa eneo hilo ambao ni Sheikh Shafi Mohammad Nina, Mudir wa Hawzat Abul _ Fadhli Al_Abbas(a.s) iliyopo Barabara ya 20 Tanga Mjini, na Ndugu Omar Salim.
Samahat Sheikh Kadhim Abbas, Mudir wa Hawzat Al_Qaim (a.t.f.s), iliyopo Barabara ya 5, Tanga Mjini, alitoa Hotuba makhsusi katika mnasaba huu na alijikita zaidi katika kudadavua kadhia ya Palestina na umuhimu wa Siku ya Quds Duniani.
Aidha, alifafanua kuhusiana na Mawayahudi na Wazayuni, na agenda za Mazayuni dhidi ya Taifa la Palestina.
Katika Hotuba yake, alidhihirisha umuhimu wa Waislamu na Watu wote huru na wapenda Haki Duniani, kuzidi kusimama pamoja na wadhulumiwa wa Palestina na kutetea Haki za watu wote wanyonge popote pale walipo Duniani.
Watu mbalimbali kutoka Jiji la Tanga walihudhuria katika Mkusanyiko huu wa kuhuisha Siku ya Kimataifa ya Quds, wakiwemo Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Kidini na Madhehebu mbalimbali.
Your Comment