Akiisisitizia kauli kwamba “uvamizi wa ubalozi wa Marekani uliimarisha uhuru wa Iran,” alisema: “Kama tukio hilo lisingetokea, leo hii Jamhuri ya Kiislamu isingekuwepo, na nchi yetu isingepata teknolojia ya makombora na nishati ya nyuklia, kwani Marekani ilikuwa inapinga maendeleo haya.”
Kikao hicho kilipambwa kwa kisomo cha Qur’an Tukufu na mashairi ya maombolezo (marsiya), ambapo walimu na wanafunzi walishiriki kwa unyenyekevu na hisia za heshima kwa mashahidi wa Karbala.