Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kufuatia kuongezeka kwa Shinikizo la Kisiasa na Kidiplomasia ndani na nje ya Lebanon kuhusu suala la kulivua silaha kundi la Hizbullah, maelfu ya Wananchi wa Lebanon wamemiminika mitaani kuonesha mshikamano wao na harakati hiyo ya mapambano.
Waandamanaji hao walijitokeza kwa wingi usiku katika mitaa ya Dahiyah ya Kusini mwa Beirut, eneo linalojulikana kuwa ngome ya Hizbullah, wakibeba bendera za harakati hiyo pamoja na picha za viongozi wake. Kwa sauti moja, walipaza kauli mbiu za kuunga mkono “haki halali ya kupambana na uvamizi wa nje,” wakisisitiza kuwa mapambano hayo ni sehemu ya heshima ya taifa la Lebanon.
Suala la kulivua silaha kundi la Hizbullah limeibuka tena hivi karibuni katika mijadala ya kisiasa ya ndani ya nchi pamoja na mashauriano ya kidiplomasia na mataifa ya nje. Wananchi wengi wamelitaja pendekezo hilo kuwa ni njama ya Kizayuni inayolenga kuondoa ngome ya mwisho ya ulinzi wa Lebanon dhidi ya uvamizi wa Israel.
Wakisambaza ujumbe wao kwa sauti na maandamano, wananchi hao wamesisitiza kuwa Hizbullah si tu harakati ya kijeshi, bali pia ni nguzo muhimu ya taifa katika ulinzi wa mipaka na heshima ya Lebanon. Kwao, wazo la kuondoa silaha za harakati hiyo ni sawa na kuiweka Lebanon mikononi mwa maadui wake.
Maandamano haya yanakuja katika kipindi ambacho hali ya kisiasa nchini Lebanon inaendelea kukumbwa na mvutano wa ndani, huku mataifa ya Magharibi yakiendelea kulishinikiza taifa hilo kulazimisha mab
Your Comment