Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Katika ujumbe wa Amir Meja Jenerali Sayyid Abdulrahim Musawi, Rais wa Makao Makuu ya Majeshi ya Ulinzi, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya mwaka wa 45 wa Utetezi Mtukufu (The Sacred Defence) imeelezwa kuwa: Wiki ya Utetezi Mtukufu inakumbusha mashahidi wa daraja ya juu na ukurasa wa dhahabu wa kusimama imara na upinzani wa wananchi wa Iran mbele ya uvamizi wa mfumo wa kibeberu. Vita vya miaka minane havikuwa tu vita vya kawaida, bali vilikuwa chuo kikuu kikubwa cha kukuza imani, azma na nguvu ya pamoja ya wananchi wa Iran; chuo ambacho wana wa nchi hii, kwa kuongozwa na Imam Khomeini (r.a) na msukumo wa Ashura, waliweza kumshinda adui aliyejihami kwa silaha za hali ya juu na kuungwa mkono na nguvu za kibeberu Mashariki na Magharibi, na hivyo kuweka mfano mpya wa uzuiaji makini, uvumilivu, kujitolea na mshikamanifu kwa ulimwengu mzima.
Katika ujumbe huo imesisitizwa kuwa: Tajiriba hii adhimu ni hazina isiyoisha kwa taifa la Iran na imetoa funzo kubwa la kimkakati; funzo la imani na kutawakali, funzo la upinzani hai na kujitegemea lililolipeleka taifa kwenye kujitosheleza kijeshi na maendeleo ya kiteknolojia, funzo la mshikamano wa kitaifa ulioonyesha kuwa mshikano wa wananchi, uongozi na jeshi unaweza kubadilisha tishio lolote kuwa fursa ya kuongeza nguvu za taifa, na funzo la kujitolea ambalo liliudhihirishia ulimwengu ushindi wa majeshi ya Kiislamu mbele ya kibeberu.
Meja Jenerali Mosavi ameongeza: Katika muendelezo wa njia ile ile, Utetezi Mtukufu ulidhihirika pia mbele ya vita vya kulazimishwa vya siku 12 na uvamizi wa wazi wa utawala wa kizayuni mchokozi na Marekani muovu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na moyo wa muqawama. Ushindi huu ulionesha tena kuwa Iran, kwa kutegemea Mwenyezi Mungu, uongozi wa hekima na ujasiri, nguvu za ndani za kijeshi na uwezo wa kikanda, inaweza kuwashinda maadui katika hatua za mwanzo kwa majibu ya ukali na yenye uzito.
Katika ujumbe huo imeelezwa: Ushindi huu ulitoa ujumbe wazi kwa maadui kuwa Iran haitabaki kimya, bali hubadilisha kila tishio kuwa nafasi ya kuonyesha nguvu zake za kitaifa, kikanda na kimataifa, na kuharibu mahesabu ya adui.
Mosavi ameongeza kuwa: Mafunzo haya ya thamani yanatuita tuimarishe ulinzi wa kila upande, kukuza teknolojia mpya za ulinzi, kuongeza uwezo wa uzuiaji na kuwa tayari kukabiliana na vita mchanganyiko hasa vya kisaikolojia na kifikra vya adui.
Amesisitiza tena: Tunawapa hakika wananchi wa Iran kuwa vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko tayari kwa majibu ya wakati muafaka, makali, ya kujutia na yaliyo zaidi ya fikra za waonevu na madhalimu wa dunia.
Katika ujumbe wake, Mosavi pia amesisitiza nafasi muhimu ya viongozi wa serikali, wananchi wenye basira na familia za askari, hususan mashahidi, majeruhi na watoa mhanga ambao ni mabendera ya utamaduni wa kujitolea na uvumilivu, na msaada wao kwa wapiganaji huipa roho mpya nguvu ya muqawama na nguvu ya taifa.
Katika sehemu nyingine ya ujumbe, Meja Jenerali Mosavi amesema: Kwa baraka za Mwenyezi Mungu na chini ya uongozi wa hekima wa Kiongozi Mkuu na Amiri Jeshi Mkuu, Ayatollah Imam Khamenei (h.f.), vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu viko tayari kama ilivyokuwa kwa nusu karne iliyopita, kubadilisha tishio lolote kuwa fursa ya maendeleo, usalama na hadhi ya Iran katika mizani ya kimkakati ya eneo na dunia.
Katika hitimisho la ujumbe wake, Mosavi amekumbusha na kuheshimu majina na harakati tukufu za mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Utetezi Mtukufu wa miaka minane na wa vita vya siku 12, hususan makamanda mashahidi Mohammad Bagheri, Gholamali Rashid na Hossein Salami na mashahidi wengine wa nguvu za Iran katika vita hivi, na kwa unyenyekevu akamuomba Mwenyezi Mungu awape wananchi wa Iran na vikosi vyake vya ulinzi msaada katika kufanikisha malengo makuu na kuelekea ustaarabu unaoandaa uongozi wa Imam wa zama.
Your Comment