Chuo Kikuu
-
Meja Jenerali Musawi: Jeshi la Ukombozi litatoa jibu lililo juu ya fikra za waonevu (waovu)
Rais wa Makao Makuu ya Majeshi ya Ulinzi wa Iran amesema: Tunawapa uhakika wananchi wa Iran wenye heshima na ushujaa kuwa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutegemea uwezo wao, ubunifu na mshangao wa kimkakati, viko tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya madhalimu na waonevu wa dunia kwa majibu ya wakati muafaka, makali, ya kujutia na yaliyo zaidi ya fikra zao.
-
Wimbi la Kukatisha Ushirikiano wa Vyuo Vikuu Duniani na Israel
Chuo Kikuu cha Amsterdam kimefuta mpango wa kubadilishana wanafunzi na Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Yerusalemu, huku Jumuiya ya Ulaya ya Wanaanthropolojia wa Kijamii ikitangaza marufuku ya aina yoyote ya ushirikiano na Israel.
-
Chuo Kikuu cha al-Mustafa (s) Dar es Salaam - Tanzania Chaandaa Kongamano la Kielimu Kuhusu: "Dakika za Mwisho za Maisha ya Mtume Muhammad (s.a.w.w)"
Mtoa Mada: Sheikh Taqi Zakariya. Tarehe: Jumamosi, 16-08-2025. Muda: Kuanzia Saa 4:00 Ask Asubuhi hadi 6:00 Mchana. Eneo: Muswalla wa Chuo Kikuu cha Al-Mustafa (s) - Dar-es-salaam. Mwaliko huu ni kwa Wote.
-
Hujjat-ul-Islam Aali: Msaada kwa wengine unarudishwa (unafidiwa) mara nyingi zaidi na Mwenyezi Mungu
Mwalimu wa chuo kikuu na shule ya kidini alieleza kuwa kusaidia na kutatua matatizo ya wengine ni chanzo cha kupata malipo mengi kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Alisisitiza kwamba sehemu ya kila mtu katika neema ya Mwenyezi Mungu inategemea uwezo wake wa kupokea, na ili kufaidika zaidi, ni lazima kuongeza uwezo huu.