Mtukufu
-
Imamu Jamaa wa Zamani wa Masjid al-Haram (Msikiti Mtukufu wa Makkah) Aachiwa Huru Baada ya Miaka 7 Gerezani Saudi Arabia
Sheikh Saleh Al-Talib mnamo mwaka 2018 katika moja ya khutba zake alipinga maonesho ya muziki (konseti) na mikusanyiko ya kijinsia iliyochanganyika, jambo lililosababisha kutoridhishwa na viongozi wa Saudia na pia shinikizo kutoka kwa taasisi za kiserikali zinazohusiana na Mamlaka Kuu ya Burudani ya Saudi Arabia, na hatimaye kusababisha kukamatwa kwake.
-
Kiongozi wa Mapinduzi atazungumza na wananchi usiku wa leo
Sambamba na Wiki Takatifu ya Ulinzi (au Wiki ya Utetezi Mtukufu - Sacred Defence), Ayatollah Khamenei atazungumza na Wananchi wa Iran na Ulimwengu mzima Usiku wa leo akidadavua masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
-
Meja Jenerali Musawi: Jeshi la Ukombozi litatoa jibu lililo juu ya fikra za waonevu (waovu)
Rais wa Makao Makuu ya Majeshi ya Ulinzi wa Iran amesema: Tunawapa uhakika wananchi wa Iran wenye heshima na ushujaa kuwa, vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu kwa kutegemea uwezo wao, ubunifu na mshangao wa kimkakati, viko tayari kukabiliana na vitisho vyovyote vya madhalimu na waonevu wa dunia kwa majibu ya wakati muafaka, makali, ya kujutia na yaliyo zaidi ya fikra zao.
-
Mawakibu (1,800) za waombolezaji yalifurika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s) kwa Mnasaba wa kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s)
Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s) Yapokea Makundi 1800 ya Waombolezaji Kutoka Ndani na Nje ya Iraq kwa Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).