25 Agosti 2025 - 09:08
Mawakibu (1,800) za waombolezaji yalifurika katika Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s) kwa Mnasaba wa kumbukumbu ya kufariki kwa Mtukufu Mtume Muhammad (s)

Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s) Yapokea Makundi 1800 ya Waombolezaji Kutoka Ndani na Nje ya Iraq kwa Kumbukumbu ya Kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlulbayt (a.s) –ABNA– Haram Tukufu ya Imam Ali (a.s), kupitia Idara ya Ulinzi na Usimamizi wa Mawakibu za Husseiniyya na Kijamii, imepokea makundi 1,800 ya waombolezaji kutoka Iraq na nje ya nchi, waliokuja kuadhimisha kumbukumbu ya kufariki kwa Mtume wa Ulimwengu wote, Muhammad (Swalla Allahu 'alayhi wa Aalihi wa Sallam), katika eneo la Kaburi -Haram Tukufu ya Amirul Mu’minin Ali bin Abi Talib (a.s).

Mkuu wa Idara ya Mawakibu za Husseiniyya na Kijamii, Khādim Hassan Zaki, alisema katika tamko lake:
"Kwa mwongozo wa Uongozi Mkuu wa Haram Takatifu ya Imam Ali (a.s) na kwa usimamizi wa idara yetu, tumepokea makundi ya waombolezaji kwa kushirikiana na idara husika. Tuliandaa mahitaji yote muhimu kwa ajili ya uendeshaji wa ibada na tukahakikisha kuwa mzunguko wa kuingia na kutoka kwa mawakibu unafanyika kwa mpangilio mzuri licha ya idadi kubwa ya mahujaji waliokuwa wakimiminika."

Zaki alieleza kuwa mpango maalum uliandaliwa kwa ajili ya mawakibu kutoka katika haram takatifu nyingine, na akasisitiza kuwa uongozi wa Haram Takatifu ya Imamu Ali (a.s) uliweka kila aina ya urahisi na msaada ili kuhakikisha kuwa ibada na kumbukumbu zinafanyika katika mazingira ya kiroho yaliyojaa utukufu.

Jitihada hizi zilihitimishwa kwa ushiriki mkubwa na maombolezo ya kugusa moyo, yaliyoonesha kwa kina upendo, heshima, na utiifu wa waumini kwa Mtume wa Allah (s.a.w.w) na nafasi yake tukufu katika nyoyo za Waislamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha