9 Oktoba 2025 - 12:23
Source: ABNA
Hamas Yatangaza Kukabidhi Orodha ya Mateka

Afisa mkuu wa Hamas alisema kuwa amekukabidhi orodha ya mateka.

Kulingana na Shirika la Habari la ABNA likinukuu tovuti ya habari ya Palestine Al-Youm, Zaher Jabareen, Mkuu wa Ofisi ya Mashahidi na Mateka wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hamas, alitangaza kuwa harakati hiyo imewasilisha orodha ya mateka wa Kipalestina kwa pande za upatanishi, kulingana na vigezo vilivyowekwa ndani ya mfumo wa makubaliano ya kusitisha mapigano na kumaliza uchokozi wa utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Gaza.

Alisema kuwa Hamas sasa inasubiri kuhitimishwa kwa makubaliano juu ya majina ili, baada ya kukamilisha uratibu na hatua husika, itangaze orodha rasmi kupitia ofisi maalum ya vyombo vya habari kwa masuala ya mateka.

Jabareen alisisitiza: Harakati ya Mapambama ya Kiislamu ya Hamas inaendelea kushikilia ahadi yake kwa mateka na familia zao zenye subira, na imeweka uhuru wa mateka wote wa Kipalestina kuwa kipaumbele chake kikuu.

Alimalizia kwa kusema: Hamas itaendelea kupigania na kufuatilia suala hili hadi mateka wa mwisho wa Kipalestina aachiliwe, na kamwe haitanyamaza mbele ya mateso na sadaka za familia zao.

Your Comment

You are replying to: .
captcha