Mufti wa Tanzani: “Ni jukumu la kila mtu kumthamini anayeithamini elimu, kwa sababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: Elimu ndio uhai wa Uislamu. Ujinga ni aibu kubwa, na hakuna anayeridhia ujinga isipokuwa punda.”
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Serena Hotel - Dar es Salaam - Tanzania leo hii imekuwa ni Simu muhimu kuadhimisha Siku ya Mufti (Mufti Day) kwa hafla maalum iliyoitwa: “Mufti Education Awards”, ambalo kwa hakika ni tukio adhimu lililolenga kuthamini na kukabidhi tuzo kwa wadau mbalimbali wa elimu nchini.
Mgeni rasmi katika hafla hii alikuwa **Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyewakilishwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa. Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa serikali, taasisi za kidini na kiserikali, pamoja na masheikh na wananchi kutoka makundi mbalimbali.
Akifafanua kuhusu tuzo hizo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally, alisema lengo kuu la *Mufti Education Awards* ni kuonyesha kwamba:
“Uislamu ni elimu na maarifa, na kamwe si ujinga.”
Aliongeza kuwa tuzo hizi zinatolewa kwa wadau wote wa elimu nchini bila kujali dini au madhehebu, ili kuwatia moyo na kuthamini mchango wao.
Aidha, Mufti alisema:
“Ni jukumu la kila mtu kumthamini anayeithamini elimu, kwa sababu Mtume Muhammad (s.a.w.w) amesema: Elimu ndio uhai wa Uislamu. Ujinga ni aibu kubwa, na hakuna anayeridhia ujinga isipokuwa punda.”
Kwa msingi huo, alibainisha kuwa aliona ni muhimu kuanzisha Tuzo za Elimu za Mufti wa Tanzania ili kuthibitisha hadharani kuwa Uislamu unapiga vita ujinga na kuhimiza maarifa.
Katika hafla hiyo, zaidi ya tuzo 30 zilitolewa kwa watu na taasisi mbalimbali za elimu kwa mujibu wa makundi na vigezo tofauti, ambapo mshindi wa kila sekta alikabidhiwa tuzo yake kwa heshima kubwa.
Your Comment