7 Oktoba 2025 - 15:22
Sheikh Ali Salman kutoka gerezani: “Kama ningekuwa huru, ningetamani kuwa pamoja na wapigania uhuru wa ‘Msafara wa Ustahimilivu (Sumud)msafara”

“Kile mnachokifanya katika msafara huu kinaheshimiwa katika dini zote, sheria zote na mila zote; ni ushahidi kuwa dhamiri ya kibinadamu bado haijafa. Harakati yenu ni fahari kwa wote sisi.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Sheikh Ali Salman, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kiislamu ya Al-Wefaq ya Bahrain, ametuma ujumbe kutoka gerezani akielezea mshikamano wake na washiriki wa Msafara wa Ustahimilivu -Sumud- (Navgan-e-Sumud), na akautaja hatua yao kuwa ni kitendo kitakatifu na cha kujivunia kwa wapenda haki kote duniani.

Katika ujumbe wake huo, Sheikh Salman aliandika:

“Salamu na heshima kwenu, enyi wapenda haki mliochagua njia ya dhamiri ya kibinadamu na mnasimama kwa ajili ya heshima ya mwanadamu katika kuwatetea wanyonge wa Gaza. Mnachokifanya kinathibitisha kuwa ubinadamu bado upo hai, na kwamba mwanadamu wa kweli hawezi kukaa kimya anapoona ukiukwaji wa utu wa binadamu mwenzake. Dhamiri safi na asili ya kibinadamu humchochea mtu kusimama kwa ajili ya kumsaidia anayedhulumiwa.

Akaongeza kuwa:

“Kile mnachokifanya katika msafara huu kinaheshimiwa katika dini zote, sheria zote na mila zote; ni ushahidi kuwa dhamiri ya kibinadamu bado haijafa. Harakati yenu ni fahari kwa wote sisi.”

Sheikh Ali Salman aliendelea kusema:

“Ninajivunia ujasiri wenu na msimamo wenu, na nina matumaini kuwa wimbi hili la mshikamano na msaada kwa wanyonge litaendelea hadi mateso yatakapoisha na mauaji ya kimbari kukoma. Kama ningekuwa nje ya gereza, ningetamani kuwa pamoja nanyi, kushiriki katika heshima hii kuu ya kibinadamu.”

Ujumbe huu umetolewa wakati ambapo mamia ya wanaharakati wa Msafara wa Ustahimilivu bado wanashikiliwa, baada ya msafara huo uliokuwa ukielekea Gaza kukamatwa na majeshi ya Israel katika maji ya kimataifa.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha