24 Septemba 2025 - 13:04
Hekalu la Chini ya Ardhi’ limechapishwa kwa Kiarabu

Katika Muktadha wa Wiki ya Utetezi Mtakatifu (Sacred Defence), tafsiri ya Kiarabu ya kitabu “Hekalu ya Chini ya Ardhi” kilichoandikwa na Ma‘sumeh Mirabutalebi, ambacho kimepambwa na (maoni ya kupongeza) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu (Ayatollah Khamenei), kimechapishwa na Dar Tamkin nchini Iraq.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-, Katika kuadhimisha Wiki ya Utetezi Mtakatifu, tafsiri ya Kiarabu ya kitabu "Ma'abadi -Hekalu- ya Chini ya Ardhi" (Al-Ma‘bad at-Taht al-Ard) kilichoandikwa na Ma‘sumeh Mirabutalebi, ambacho kimepambwa na Taqridh (maoni ya kimaandishi ya kusifu na kupongeza) ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, kimechapishwa na Dar Tamkin nchini Iraq.

Toleo la Kifarsi la kitabu hiki, ambacho awali kilichapishwa na Chapisho la Ketabe Jamkaran, kinaeleza hadithi ya moja ya sehemu zisizoangaziwa sana za Vita vya Kujihami Kutakatifu (vita vya Iraq dhidi ya Iran).

Kisa cha kitabu hiki kinatokea katika miaka ya vita vya kulazimishwa, wakati ambapo tatizo gumu linaloathiri operesheni za kijeshi lilitokea—tatizo hilo likatatuliwa na wachimba-mahandaki wa mji wa Yazd. Hii ni simulizi ya ushujaa wa kimya wa watu wa kawaida waliotoa mchango mkubwa bila kutambulika hadharani.

Hekalu la Chini ya Ardhi’ limechapishwa kwa Kiarabu

Kabla ya hapo, Katika tukio la 18 la kuheshimu kuthamini fasihi ya jihad na Muqawama (Muqawama = Upinzani wa kishujaa dhidi ya udhalimu), ambalo lilijikita kwenye ushujaa wa wachimba-mahandaki wa Yazd, Taqridh (تقريظ) ya Ayatollah Khamenei kuhusu riwaya ya "Ma'abadi ya Chini ya Ardhi" (Ma‘bad-e Zīr-e Zamīn) ilichapishwa.
Riwaya hii imeandikwa kwa msingi wa maisha ya Shahidi Gholamhossein Ra’eyat Rokanabadi, mzaliwa wa kijiji cha Roknabād katika mji wa Meybod, jimbo la Yazd.

Taqridh ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi (Taqridh: Ni Maandishi ya sifa au pongezi kuhusu kitabu fulani, yanayoandikwa na mtu maarufu, mwanazuoni au kiongozi wa kidini)


Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

“Mada ya riwaya hii ni mpya na ya ubunifu. Uandishi wake pia ni mtamu na wa kuvutia. Kuingilia maeneo ya pembeni lakini muhimu na yenye athari kubwa katika utetezi mtakatifu ni jambo la lazima, na mwandishi wa riwaya hii fasaha amelitimiza kwa mafanikio. Kutumia wachimba-mahandaki wa Yazd ni jambo ambalo Shahidi Sayyad Shirazi aliwahi kulitaja mara kadhaa, nasi tulikuwa tumelisikia, lakini umuhimu, umahiri na ugumu wa kazi hiyo, kama ilivyofafanuliwa ndani ya kitabu hiki, haukuwa bayana kwetu wala kwa watu wengine wa aina yetu. Rehema na radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya wasanii hawa wa kishujaa waliokuwa na koleo mikononi.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha