21 Machi 2025 - 15:47
Wamarekani wanapaswa kujua: Vitisho havipeleki popote; Kofi kali la usoni ni jibu la uovu wowote

Ayatollah Khamenei amesisitiza kuwa, Wamarekani wanapaswa kujua kwamba kamwe hawatafika popote kwa vitisho dhidi ya Iran na akasema: Wao na wengine wanapaswa kujua kwamba iwapo watafanya jambo lolote ovu kwa Taifa la Iran, watapigwa kofi kali.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA-, katika siku ya kwanza ya mwaka mpya, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika kikao chake na maelfu ya watu wa matabaka mbalimbali, ameitaja mila (na desturi) ya Iran ya kuanza mwaka mpya kwa sala na dua na kukusanyika katika vituo vilivyobarikiwa kuwa ni ishara ya mtazamo wa kiroho ya kimaanawi wa Taifa hili kuhusu (siku ya mwaka mpya ya) Nowruz, na akaeleza athari za sala, dua na subira katika ushindi mkubwa wa Mrengo wa Kulia katika kipindi chote cha historia, ambapo aliuhesabu mwaka ulioisha (na kupita) kuwa mwaka wa subira, uvumilivu na udhihirisho wa nguvu za kiroho za watu wa Iran, na kulitakia heri ya mwaka mpya Taifa lote, huku akibainisha wajibu wa Wananchi na Serikali katika kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu mpya (wa 1404 Hijria Shamsia) yaani "Uwekezaji kwa ajili ya uzalishaji, " na kuboresha hali ya uchumi na maisha.

Ayatollah Khamenei ameashiria pia chukio la jumla la mataifa ya ulimwengu kwa jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni na kuiona lugha ya vitisho kuwa ni lugha isiyo na matunda na iliyofeli mbele ya Taifa kubwa la Iran na kuongeza: Mataifa na vituo vya Mapambano ya Muqawamah (Upinzani) likiwemo Taifa la Palestina, Lebanon na Yemen kwa msukumo wao wa ndani na imani, wanajishughulisha na kusimama dhidi ya utawala muovu na potovu wa Kizayuni.

Ayatollah Khamenei akiashiria juu ya gharama za mara kwa mara (za muda wote) za mrengo wa haki katika mapambano yake ya Muqawamah dhidi ya upande wa batili amesema kuwa: Ni lazima tuyaangalie matukio ya mwaka ulioisha wa 1403 (Hijria Shamsia) kwa mtazamo kwamba katika mapambano kati ya haki na batili, hakika ushindi unatokana na mrengo wa haki, lakini kwa njia hii, hatuna budi kulipa gharama, kama ilivyokuwa na ilivyojiri Sunna hii ya Mwenyezi Mungu katika ulinzi mtakatifu (katika vita vya miaka 8 dhidi ya Iran).

Akirejelea kupoteza shakhsia kubwa wa Iran na Lebanon katika matukio ya mwaka ulioisha wa (1403), ametaja kushindwa kwa maadui hususan utawala ghasibu, fasiki, dhali na muovu wa Kizayuni kuwa ni hatimaya ya kustahimili matukio haya machungu na "kudumu katika kutafuta - na kutegemea - msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu" na akasisitiza: Katika mwaka mgumu wa 1403, nguvu ya kiroho, uvumilivu, ujasiri na ushujaa wa Taifa ulionyesha mwangaza mkali.

Hadhrat Ayatollah Khamenei ameorodhesha tukio kubwa la (mazishi) kuusindikiza mwili wa Shahidi Raisi, mahudhurio ya nadra (na yasiyokuwa na kifani) katika Sala ya Ijumaa ya Ushindi licha ya uwepo wa vitisho vya adui, kushiriki kwa hamasa katika uchaguzi wa Rais na mazishi yenye maana kubwa ya Shahidi Ismail Haniyeh na majenerali wengine waliouawa Shahidi katika Mashambulizi ya utawala wa Kizayuni, na kuongeza kuwa: Maandamano ya kihistoria ya tarehe 22 Bahman (sawa na 11 Februari - ya kuadhimisha Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979), yalikuwa kilele cha mchakato huo ambao ulifichua uaminifu wa Taifa la Iran kwa Mapinduzi ya Kiislamu na kudhihirisha mapenzi (na maslahi) ya watu juu ya Jamhuri ya Kiislamu mbele ya wanafiki wote, na kulifanya Taifa la Iran lijulikane kwa Walimwengu wote.

Wamarekani wanapaswa kujua: Vitisho havipeleki popote; Kofi kali la usoni ni jibu la uovu wowote

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, alitoa hoja kadhaa kuhusu kauli nyingi za maafisa wa Marekani

Ayatollah Khamenei amesisitiza kuwa, Wamarekani wanapaswa kujua kwamba kamwe hawatafika popote na vitisho vyao dhidi ya Iran na akasema: Wao na wengine wanapaswa kujua kwamba iwapo watalifanya jambo lolote ovu dhidi ya Taifa la Iran, watapigwa kofi kali la usoni.

Katika kubainisha nukta nyingine, ameitaja tafsiri ya wanasiasa wa Marekani na Ulaya kuhusiana na vituo vya Mapambano ya Muqawamah kuwa ni vikosi vya kijeshi vya wakala wa Iran kuwahilo  ni kosa kubwa, na ni kuyadhalilisha makundi hayo, na akaongeza: Nini maana ya wakala (au kwa niaba ya)? Wananchi wa Yemen na vitovu vya Mapambano ya Muqawamah (Upinzani) katika eneo hili la kikanda wana msukumo wa ndani na imani wa kusimama dhidi ya Wazayuni, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haihitaji naibu (wakala), na maoni yetu na maoni yao yanajulikana.

Kiongozi wa Mapinduzi ameutaja ustahamilivu, subira na Mapambano ya Muqawama dhidi ya uovu na ukatili wa utawala haram na ghasibu (nyakuzi) wa Kizayuni kuwa ni jambo ambalo limekita mizizi katika eneo la kikanda, na kuongeza: Mwanzoni mwa unyakuzi wa Palestina, moja ya nchi zilizokuwa katika mstari wa kukabili dhulma hiyo ni Yemen, mtawala wa siku hiyo alipokuwa katika kushiriki kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Kimataifa alipinga wazi wazi unyakuzi wa Palestina.

Ayatollah Khamenei akiashiria kuenea kwa maandamano ya kupinga jinai za utawala katili wa Kizayuni ya mataifa yasiyo ya Kiislamu na maandamano ya hadhara kubwa na ya Wanafunzi huko Marekani na nchi za Ulaya, amesema: Viongozi wa nchi za Magharibi hawataki kuona ukweli huu na kuelewa misimamo ya mataifa yao; Kwa hiyo, wanaenda kufanya kazi kama vile kukata bajeti ya chuo kikuu ambayo wanafunzi wake wameonyesha kusapoti Palestina, ambapo bila shaka hilo ni dhihirisho la madai yao (feki na ya uongo) katika uwanja wa Usambazaji Huru wa Habari, Uliberali na Haki za Binadamu.

Akisisitiza upinzani wa mataifa dhidi ya maovu ya utawala wa Kizayuni na kuupinga kwa kila njia, ameongeza kuwa: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nayo imesimama kidete kukabiliana na maovu hayo na imeeleza wazi na bayana msimamo na mbinu yake ya kawaida kabisa kwamba inawaunga mkono wapiganaji wa Palestina na Lebanon wanaozihami nchi zao.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kwa mara nyingine tena katika kujibu vitisho vya wenye nia mbaya dhidi ya Iran: Hatujawahi kuanzisha mzozo na mgogoro na huyu na yule, lakini mtu akianzisha mgogoro na mzozo kwa nia mbaya (dhidi yetu), ajue kwamba atapigwa makofi makali mno ya usoni.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha