Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA -; AyatOllah Khamenei, akizungumzia mfanano wa mwanzo wa mwaka mpya na Mikesha ya Nyusiku za Lailatul-Qadr na siku za kuuawa Shahidi Imam Ali (a.s), ameelezea matumaini yake kwamba Baraka za Mikesha ya Lailatul-Qadr na kumzingatia Mwenyezi Mungu kwa Waumini yatajumuisha hali ya watu wote wapenzi wa Iran na wale wote ambao mwaka wao mpya unaanza na Nowruz.
Aliuchukulia mwaka wa 1403 (Hijri Shamsi) ulioisha kuwa ulikuwa ni mwaka uliojaa matukio yanayofuatana na yanayofanana na matukio ya miaka ya 60, na ulioambatana na dhiki, ugumu na matatizo kwa watu na akasema: Kuuawa Shahidi idadi kadhaa ya washauri wa Kiiran huko Damascus, kuuawa Shahidi Sayyid Raisi, Rais mpendwa wa Taifa la Iran, na baada ya matukio hayo machungu ndani ya Tehran na Lebanon, yalisababisha Taifa la Iran na Umma wa Kiislamu kupoteza mambo yenye thamani kubwa kwa mwaka huu.
Kiongozi wa Mapinduzi aliorodhesha shinikizo la shida za kiuchumi na ugumu wa maisha, haswa katika nusu ya pili ya mwaka, kuwa ni kati ya matukio mengine ya Mwaka wa 1403 (Hijri Shamsi), na akabainisha: Katika kukabiliana na matatizo hayo, jambo kubwa na la ajabu lilijitokeza, yaani, nguvu ya nia (irada) na roho ya kimaanawi ya Taifa la Iran na umoja wao, na maandalizi yao ya hali ya juu yalionekana, ambayo dhihirisho lake la kwanza lilikuwa katika kukabiliana na kupotea kwa Rais wa Jamhuri, na kauli mbiu na ari ya juu ya Wananchi katika msafara huo mkubwa, ambao ulionyesha kwamba msiba huu mzito kwa Taifa, hauwezi kuleta maafa makubwa kwa Taifa.
Amekutaja kufanyika haraka kwa uchaguzi wa Rais (mpya) ndani ya muda wa mwisho wa kisheria na kuiondoa nchi katika ombwe la utawala kwa kumchagua Rais mpya na kuunda Serikali kuwa ni dhihirisho jingine la moyo na uwezo wa hali ya juu wa kiroho wa Wairan, na katika kueleza eneo jingine la udhihirisho wa nguvu ya kiroho ya Taifa amesema: Katika kukabiliana na matatizo ya watu wa Lebanon na Palestina, Taifa la Iran lilituma mafuriko makubwa ya misaada ya umma kwa ndugu zake kaka na dada wa kidini huko Lebanon na Palestina.
Ayatollah Khamenei alizingatia michango ya kustaajabisha ya Wananchi kwa Muqawamah hususan mchango mkubwa wa Dhahabu uliotolewa na Wanawake wa Iran kuwa ni moja ya matukio ya kudumu na yasiyosahaulika katika historia ya nchi, na akasema: Nguvu ya irada na azma ya Taifa na nguvu ya roho ya kimaanawi ya watu ni tunu yenye thamani kubwa kwa mustakbali na muda wote wa Iran pendwa, na hilo litapelekea kuendelea kwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya nchi hii.
Katika sehemu nyingine ya ujumbe wa Nowruz, Kiongozi wa Mapinduzi, akimaanisha kuutaja Mwaka wa 1403 Hijria Shamsia kama Mwaka wa ""Ustawi wa Uzalishaji kwa Kushirikisha Wananchi", aliyataja matukio ya mwaka huu uliopita kwamba, licha ya juhudi za Serikali, Wananchi na Sekta binafsi, matukio hayo ya mwaka uliopita yalizuia utimilifu kamili wa kauli mbiu hii, na akaongeza: Kwa hiyo, mwaka huu kauli mbiu na suala kuu bado ni la kiuchumi na kuangalia zaidi suala la uwekezaji, kwa sababu ustawi wa uzalishaji na kutatua matatizo ya maisha (ya watu) kunategemea utambuzi wa Uwekezaji katika Uzalishaji.
Akisisitiza nafasi ya Serikali kuwa msingi wa uwekezaji wa Wananchi katika Sekta ya uzalishaji alisema: Ni kweli pale ambapo watu hawana ari wala uwezo wa kuwekeza, Serikali inaweza kuingia uwanjani na kuwekeza kama mbadala na si mshindani wa Wananchi.
Hadhrat Ayatollah Khamenei aliona ni muhimu kufikia uwekezaji katika uzalishaji kwa kujenga dhamira na hamasa kubwa ndani ya Serikali na Wananchi, na akasema: Kazi ya Serikali ni kuweka msingi na kuondoa vikwazo vya uzalishaji kwenye kazi za watu, kuileta mitaji yao midogo na mikubwa katika njia ya uzalishaji, kwa hali hiyo miji mikuu haitaenda tena kwenye vitu vyenye madhara kama sarafu na dhahabu, na katika uwanja huu, Benki kuu na Serikali wana jukumu lenye athari zaidi.
Kwa utangulizi huo, Kiongozi huyo wa Mapinduzi alisoma kauli mbiu ya mwaka mpya wa 1404 Hijria Shamsia kuwa ni “Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji” na kueleza matumaini yake kuwa kwa mipango ya Serikali na ushirikishwaji wa Wananchi, utapatikana mwanya katika suala la kujitafutia riziki.
Katika sehemu ya mwisho ya hotuba yake, Ayatollah Khamenei ameutaja uvamizi upya wa utawala ghasibu wa Kizayuni huko Ghaza kuwa ni jinai kubwa na mbaya sana na akasisitiza: Suala hili ni suala la Umma wa Kiislamu, hivyo Ummah wote unapaswa kuweka kando tofauti zao na kusimama kidete kukabiliana na jinai hizi. Pia, watu wote walio huru duniani, wakiwemo wa Ulaya na Marekani, lazima wakabiliane na hatua hiyo ya kisaliti na ya maafa na kuzuia mauaji ya watoto, uharibifu wa nyumba na watu kuyahama makazi yao.
Huku akisisitiza kuwa, Marekani inashiriki dhima ya maafa hayo na kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya kisiasa, jinai hiyo imefanywa kwa amri ya Marekani au kwa idhini yake, amesema: Matukio ya Yemen na mashambulizi dhidi ya watu na raia wa Yemen ni jinai nyingine inayopaswa kuzuiwa.
Mwishoni mwa hotuba yake, Kiongozi wa Mapinduzi aliutakia Umma wa Kiislamu kheri na ushindi, pamoja na kuendelea kwa furaha, kuridhika, mafanikio na umoja kamili wa Taifa la Iran hadi mwisho wa mwaka huu, na kueleza matumaini yake kwamba Moyo Mtukufu wa Hadhrat Walii al-Asr (a.t.f.s) na roho safi ya Imam Mtukufu na Mashahidi, zitaridhika na kuwaridhia Wananchi wa Iran.
Your Comment