Nowruz
-
Tutajitahidi kufanya thamani yetu kuwa bora zaidi na ya juu zaidi kuliko ilivyo kwa sasa katika mzunguko mpya wa nyakati
Akisema kwamba Nowruz na na Nyusiku za Lailat al-Qadr ni miale miwili ya nuru moja na madhihirisho mawili ya ukweli uleule (ulio sawa), Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tunakesha katika usiku huu ili kuwa Wanadamu wapya kwa kuzisafisha nafsi zetu na kufikia hatima (makadirio) yetu katika siku mpya, lakini hatima (makadirio) yetu na nchi yetu si mahali hapa tuliposimama; Uthamani wetu ni wa juu kuliko hali yetu ya sasa.
-
Ujumbe wa Waziri wa Miongozo katika hafla ya Nowruz na Nyusiku za Lailat -ul- Qadr
Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, kwa mnasaba wa kuwasili kwa Nowruz ya mwaka mpya wa 1404 unaosadifiana na Mikesha ya Nyusiku Tukufu za Lailatul Qadr, katika ujumbe wake, alizingatia fahari ya Iran kuwa ni faraja kwa maisha ya kila mmoja wa Wananchi.
-
Ujumbe wa Nowruz wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa Mnasaba wa Mwaka Mpya
Mwaka 1404, ni Mwaka wa "Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji"
Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa mwanzo wa mwaka mpya wa 1404 Hijria Shamsia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya kuwa ni mwaka wa "Uwekezaji kwa ajili ya Uzalishaji".