20 Machi 2025 - 16:37
Tutajitahidi kufanya thamani yetu kuwa bora zaidi na ya juu zaidi kuliko ilivyo kwa sasa katika mzunguko mpya wa nyakati

Akisema kwamba Nowruz na na Nyusiku za Lailat al-Qadr ni miale miwili ya nuru moja na madhihirisho mawili ya ukweli uleule (ulio sawa), Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tunakesha katika usiku huu ili kuwa Wanadamu wapya kwa kuzisafisha nafsi zetu na kufikia hatima (makadirio) yetu katika siku mpya, lakini hatima (makadirio) yetu na nchi yetu si mahali hapa tuliposimama; Uthamani wetu ni wa juu kuliko hali yetu ya sasa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Dk.Masoud Pezeshkian amesema katika ujumbe wake wa Nowruz kwa mnasaba wa Mwaka Mpya na Nowruz wa 1404: Mwanzoni mwa mzunguko mpya wa nyakati, tutaweka thamani yetu kuwa bora zaidi na ya juu zaidi na ya heshima zaidi kuliko wakati tuliokuwa nao wa sasa, na tumeazimia kwamba kwa uelewa na mshikamano wetu, tutaitoa na kuiweka Iran yetu pendwa mbali na ubaya, uchafu na dhulma kwa itikadi na imani yetu na kwa nia na azma yenu enyi watu wapendwa, na hatutaacha juhudi zozote za kufikia hilo.

Ifuatayo ni sehemu ya nakala ya ujumbe wa Rais wa Iran:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Ewe Mwenye kubadilisha nyoyo na macho

Ewe Mola Mlezi Mwenye kuendesha Usiku na Mchana

Ewe Mwenye kugeuza (kubadilisha) Mwaka na Hali

Badilisha hali yetu kuwa bora zaidi.

Kwa kuwadia kwa mwaka mpya na kuwasili kwa nyusiku mpya, Nyusiku za Lailatul al-Qadr, ningependa kuwapongeza wairan wote nchini kwa Eid ya Nowruz na wale wote waliopo nje ya nchi, na kila mahali ulimwenguni, na vile vile nchi majirani na watu wote wa eneo la kikanda, na ninawatakia nyote kwa ujumla amani, urafiki na furaha.

Nowruz na Nyusiku Tukufu za Lailatul Qadr ni miale miwili ya nuru moja na ni madhihirisho mawili ya ukweli ulio sawa; Ukweli wa mabadiliko na mwanga wa mabadiliko yanayotokea katika hatima (makadirio) yetu.

Quran ni Kitabu cha uzima, ni Kitabu cha kuwatoa watu gizani kuwapeleka kwenye nuru, kutoka kwenye ujinga hadi kwenye mwanga, kutoka kwenye ulegevu na uvivu hadi kwenye juhudi na nguvu na kusimamisha haki na uadilifu katika jamii, na leo hii pamoja na matatizo yote yanayotukabili nchini, katika Mikesha ya Nyusiku za Lailatul Qadr, ni lazima tuamue kuwa popote pale tulipo, tutabadili mkondo na njia katika uelekeo wake, na kisha Qur'an iwe ndio muongozo wetu wa kuifikia, na Malaika na roho zote zitakuwa pamoja nasi, mpaka tuondoe pazia jeusi na kufikia alfajiri na nuru.

Kwa mtazamo huo huo, Nowruz itafungua siku mpya na msimu mpya mbele yetu, na kama ilivyotajwa katika amri ya Kiongozi wetu Ali (amani iwe juu yake) kwa Malik al-Ashtar: (و لا تنقض سنّة صالحة عمل بها صدور هذه الأمّة، و اجتمعت بها الألفة، و صلحت عليها الرّعيّة) / "Usibadilishe Sunna nzuri na bora walizoziasisi na kuzifuata watangulizi wa Umma huu, na watu wanahisi hali zao zinakuwa nzuri na bora kwa sababu yake, na zinasababisha ukaribu, mshikamano na urafiki wa watu, usivunje sunna hizo na bila shaka yoyote hazivunjiki, Nowruz ni miongoni mwa Sunna hizi nzuri zilizotoka katika historia ya Iran na zimethibitishwa na Dini Tukufu ya Kiislamu.

Tunakesha katika Nyusiku hizi Tukufu za Lailatul Qadr ili kuwa Wanadamu wapya kwa kuzitakasa nafsi zetu na kufikia hatima (makadirio) yetu katika siku mpya, lakini hatima (makadirio) yetu na nchi yetu sio mahali hapa tuliposimama; Uthamani wetu ni wa juu kuliko hali yetu ya sasa. 

Nyusiku za Lailat Al-Qadr ni Nyusiku Tukufu, kwa upande mmoja, na ni Nyusiku za furaha ya kiroho inayosababishwa na kusikia sauti ya Mwenyezi Mungu na kuteremshwa kwa neno la Mwenyezi Mungu na Qur'an Tukufu, na kwa upande mwingine, ni Nyusiku za maombolezo ya Kuuawa Shahidi Sayyidna Ali (amani iwe juu yake), ambaye alikuwa ni Sauti ya uadilifu wa Mwanadamu. Imam Ali (aamani iwe juu yake), alifanya kazi kwa muda wa miaka 25 ya ukimya kwa ajili ya umoja, na kwa ajili ya kusimamisha Serikali ya Uadilifu, na hatimaye akawa Shahidi wa Haki, lakini Uadilifu wa Imam Ali (amani iwe juu yake) ulikuwa wa daraja ya juu kiasi kwamba hadi wakati wa Kifo chake cha Kishahidi, aliamuru kumtendea Haki muuaji wake. Kama alivyosema Shahriar katika kauli yake:

"Isipokuwa Ali ambaye anasema, kwa yule kijana aliyeniua *** Na kwa kuwa kwa sasa amekuwa ni mateka kwenu, basi kuweni na subira na mateka wenu".

Ulimwengu na Ubinadamu daima umekuwa na kiu ya (kupata) Haki kama hiyo, na hii ndiyo sehemu inayokosekana (leo hii) ya asili ya Mwanadamu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha