Pezeshkian
-
Pezeshkian: Iran daima imesimama imara mbele ya Dhoruba za Historia / Watenda jinai ambao mwenendo wao ni kuua watoto, hawastahili kuitwa Binadamu
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa Iran, hii ndiyo ustaarabu wa kale zaidi unaoendelea duniani, na daima imesimama imara mbele ya dhoruba za historia. Taifa hili, kwa roho kuu na azma isiyokoma, mara nyingi limethibitisha kwamba haliinamii mbele ya wavamizi; na leo pia limesimama kwa heshima mbele ya wanyakuzi, likitegemea nguvu ya imani na mshikamano wa kitaifa
-
Tutajitahidi kufanya thamani yetu kuwa bora zaidi na ya juu zaidi kuliko ilivyo kwa sasa katika mzunguko mpya wa nyakati
Akisema kwamba Nowruz na na Nyusiku za Lailat al-Qadr ni miale miwili ya nuru moja na madhihirisho mawili ya ukweli uleule (ulio sawa), Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema: Tunakesha katika usiku huu ili kuwa Wanadamu wapya kwa kuzisafisha nafsi zetu na kufikia hatima (makadirio) yetu katika siku mpya, lakini hatima (makadirio) yetu na nchi yetu si mahali hapa tuliposimama; Uthamani wetu ni wa juu kuliko hali yetu ya sasa.
-
Dk. Pezeshkian: Ikiwa mwongozo wa Qur'an hauonekani katika matendo na maisha yetu, basi tunapaswa kufikiria upya tabia zetu.
Akisisitiza umuhimu wa kuunganisha maarifa ya Qur'an na matendo ya kijamii, Rais wa Iran amesema: Tatizo kubwa ni pengo kati ya kuijua na kuitekeleza Qur'an. Tunadai kuwa Qur’an inatuonyesha njia ya uongofu na inamfikisha Mwanadamu katika kilele cha juu zaidi, lakini ikiwa kivitendo hakuna dalili ya mwongozo huu inayoweza kuonekana katika maisha yetu ya kibinafsi na ya kijamii, basi kwa hakika tunapaswa kuangalia upya tabia zetu.