20 Machi 2025 - 15:25
Ujumbe wa Waziri wa Miongozo katika hafla ya Nowruz na Nyusiku za Lailat -ul- Qadr

Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, kwa mnasaba wa kuwasili kwa Nowruz ya mwaka mpya wa 1404 unaosadifiana na Mikesha ya Nyusiku Tukufu za Lailatul Qadr, katika ujumbe wake, alizingatia fahari ya Iran kuwa ni faraja kwa maisha ya kila mmoja wa Wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (AS) - ABNA -, Sayyid Abbas Salehi, Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu, alitoa ujumbe kwa mnasaba wa kuwasili kwa Eid ya Nowruz iliyosadifiana na Mikesha ya Lailatul Qadr na Kuuawa Shahidi Amir al-Mu'minin Ali bin Abi Talib (amani iwe juu yake).

Nakala ya ujumbe wa Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu inasema kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mungu wa Chemchemi na Msamaha

Mwaka huu, Nowruz inakuja kwenye kizingiti tofauti kuliko kawaida; Ambapo Nyusiku za Makadirio, Nyusiku za baraka za kuamua hatima ya Wanadamu, zimeambatana na wakati wa Mwaka Mpya.

Katika sanjari hii ya kustaajabisha, kwa upande mmoja, nyakati za usiku ambazo milango ya rehema isiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu inafunguliwa, na Malaika wanashuka juu ya ardhi, na kwa upande mwingine, Nowruz, ambayo ina ahadi ya upya na kuondolewa kwa uzee (au uchakavu) katika moyo.

Sasa kwa vile mwaka mpya unakuja, kuliko wakati mwingine wowote, inafaa kuleta mioyo yetu pamoja na kuiombea Iran na Wairan katika nyusiku hizi pendwa (za Lailatul - Qadr).

Tuombe kwa ajili ya nchi yetu ili iweze kuibuka na kutoka kwenye heka heka za wakati, vumbi la matatizo litulie, na uadui ufifie na Iran ichukue hatua zaidi katika njia ya ukuaji na maendeleo. Bila shaka, fahari ya Iran itarahisisha maisha kwa kila raia.

Katika mikesha hii ya neema na siku za Nowruz, tunaomba kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya kufanywa upya Iran, kwa ajili ya ushindi wa Iran, na kwa ajili ya mwaka ujao kuwa mwaka wa Kiutamaduni, Kiuchumi na Kijamii na wenye Matunda kwa watu wa ardhi hii.

Nakutakieni Siku yenye Furaha na Baraka ya Nowruz, Dua na Maombi yenu yawe ni yenye kujibiwa, na makadirio (hatima) yenu iwe katika njia ya Kheri na Baraka.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha