Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-BNayt (as) -ABNA- Bango lililosimikwa Barabarani huko Mumbai (Bombay) - India lina ujumbe kuhusiana na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, na linasomeka hivi: "Tuna bahati kuwa tumezaliwa wakati wako na kukuona kwa karibu, hatukuishia tu kusoma hadithi za ujasiri na ushujaa kwenye vitabu."
Katika bango hilo lenye picha ya Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, upande wa kushoto, anayeonekana katika picha ni Mwanasiasa Mashuhuri Msunni huko Mumbai. Kauli hii katika kumsifu na kumsapoti Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, inatukumbusha kauli maarufu na mashuhuri ya Imam Khomeini (RA) aliposema: "Vita dhidi yetu ni baraka kwetu".
Your Comment