Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Abbas Ramadhan, leo Jumatano, tarehe 22 Julai 2026, ameongoza kikao maalum cha Baraza la Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za BAKWATA Mkoa, zilizopo Mtaa wa Aggrey, Dar es Salaam.
Miongoni mwa ajenda kuu za kikao hicho ilikuwa ni kupitia na kuchuja majina ya wagombea wa uongozi wa Baraza la Masheikh katika ngazi ya wilaya, ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kuandaa uongozi wa baraza hilo katika ngazi mbalimbali.
Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uongozi, ushirikiano na utendaji wa Baraza la Masheikh katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Maoni yako