Mohsen Rezaei, Jenerali mstaafu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na mmoja wa viongozi mashuhuri wa kijeshi na kisiasa nchini Iran, ameteuliwa kuwa: Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Uteuzi huo unamrudisha mwanajeshi huyo mwenye uzoefu mkubwa katika nafasi nyeti ya kuratibu masuala ya usalama wa taifa wakati Iran ikiendelea kuandamwa na changamoto kubwa za kiusalama na kisiasa kutoka kwa maadui Marekani na Israel.
Jake Lang, mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa Seneti ya Florida na mmoja wa wafuasi wakubwa wa Trump, baada ya kushindwa kutekeleza kitendo cha kuchoma Qur’ani huko Dearborn, jimbo la Michigan, na kuingia katika makabiliano na waandamanaji, amewasilisha kesi ya dola milioni 200 akimshutumu Meya Mwislamu wa jiji hilo na polisi wa eneo hilo kwa “kutompa ulinzi.”
Hapo awali, picha zilizochukuliwa na waandishi wa habari huru na vyombo kama Reuters na Anadolu zilionyesha kwamba Lang alijaribu kuchoma nakala ya Qur’ani kwa kutumia kimiminika cha kuwasha moto, lakini alikabiliwa mara moja na mpinga-maandamano aliyemtibua kabla ya kufanya kitendo hicho.