24 Agosti 2025 - 15:38
“Haiwezekani kuupiga magoti Umma wa Iran na Mfumo wa Kiislamu kupitia vita"

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Shahada ya Imam Ridha (a.s), amesema: "Umma wa Iran na Mfumo wa Kiislamu hauwezi kupigwa magoti kwa vita na kulazimishwa kusalimu amri"

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Maadhimisho ya Shahada ya Imam Ali bin Musa al-Ridha (a.s) yalifanyika asubuhi ya leo, Jumapili, tarehe 24 Agosti, 2025, katika Husseiniyya ya Imam Khomeini (r.a) kwa kuhudhuriwa na Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatollah Khamenei.

Katika hotuba yake mbele ya maelfu ya wananchi kutoka tabaka mbalimbali, Ayatullah Khamenei alibainisha mambo muhimu kuhusu masuala ya kisasa na kusisitiza kuwa: “Maadui wa Iran, kutokana na uthabiti na mshikamano madhubuti wa wananchi, viongozi na majeshi ya ulinzi, pamoja na kushindwa kwao vibaya katika mashambulizi ya kijeshi, wameelewa kuwa haiwezekani kuilazimisha Iran kupitia vita. Kwa sababu hiyo, sasa wanajaribu kufanikisha lengo hilo kwa kuunda migawanyiko ya ndani.”

Akasema: “Ndiyo maana ni jukumu la wananchi wote, viongozi na wenye kalamu kulinda na kuimarisha ngao ya kitaifa ya mshikamano mtakatifu na wa heshima kubwa.”

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliongeza akisema: “Wote tunapaswa kumuunga mkono Rais mwenye bidii na viongozi wa serikali wanaotoa huduma kwa wananchi.”

“Haiwezekani kuupiga magoti Umma wa Iran na Mfumo wa Kiislamu kupitia vita"

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha