Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna - Huduma ya Kurasa za Utamaduni
Sambamba na Sala adhimu ya Eid al-Fitr ilipokuwa ikisaliwa na kutekelezwa kote nchini, maelfu ya waumini wa mji wa Tehran walisali Sala ya Eid al-Fitr asubuhi ya Jumatatu, 31 Machi, 2025, chini ya Uimam / Uongozi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, katika Msikiti wa Imam Khomeini (RA).
Fahirisi ya maneno (Hotuba) yake katika Khutba mbili za Sala ya Eid al-Fitr inawasilishwa sehemu hii kwa muhtasarai kwa wasomaji wa Abna kama ifuatavyo:
Utawala wa Kizayuni ni (Mawakala) kikosi kiwakilishi cha Wakoloni katika eneo hili la kikanda
* Ramadhan:
- Ni moja ya Baraka kuu za Mwenyezi Mungu.
- Ni jambo la Tauhidi (Kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja).
- Ni fursa iliyotolewa na Mola kwa waja Wake kwa ajili ya Ucha Mungu na kutengeneza ukaribu wao na Mwenyezi Mungu, utakaso wa nafsi zao na roho zao, na kujihuisha upya kimaanawi [kiroho].
- Saumu, ukaribu na Qur'an, mikesha ya nyusiku zenye baraka za Lailatul-Qadr, sala na dua ni fursa adhimu na za kumjenga Mwanadamu zilizopo ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
* Uchungu kamili kwa Umma wa Kiislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani:
- Kuendelea kwa jina na mauaji ya halaiki na mauaji ya watoto wachanga yanayofanywa na utawala ghasibu wa Kizayuni huko Gaza na Lebanon kulisababisha machungu ya Umma wa Kiislamu katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
- Uhalifu huu ulifanyika katika kivuli cha kuendelea kwa misaada na uungaji mkono wa Marekani kwa genge la uhalifu linaloiteka na kuikalia kimabavu Palestina.
* Utawala wa Kizayuni ni Kikosi Kiwakilishi cha Wakoloni katika eneo hili la kikanda:
- Watu wa Magharibi mara kwa mara wanashutumu mataifa shujaa na vijana wenye bidii (wapambanaji katika jihadi tukufu) wa eneo hili la kikanda kuwa ni wawakilishi (mawakala).
- Lakini ni wazi kabisa kwamba kikosi pekee cha wakala katika eneo hili la kikanda ni utawala ghasibu na wa kifisadi wa kizayuni unaoendelea na kukamilisha mpango wa nchi zilizolikoloni eneo hili (la Mashariki ya Kati) baada ya Vita vya Kidunia kwa uchomaji moto, mauaji ya halaiki na uchokozi dhidi ya nchi zingine.
* Kimya cha Wamagharibi mbele ya jinai za utawala wa Kizayuni:
- Watu wale wale ambao kwa maneno yao wanaita utetezi wa mataifa kwa haki zao na ardhi zao kuwa ni ugaidi na uhalifu, lakini ajabu wanachokifanya ima wanafumbia macho mauaji ya halaiki ya utawala haram wa kizayuni, au wanasaidia kabia kuanzisha na kuendeleza vitendo vya kigaidi vya Wazayuni.
- Mauaji ya watu kama vile Abu Jihad, Fat'hi Shaqqa'qi, Ahmed Yassin na Imad Mughniyeh katika nchi tofauti yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni, na vile vile na mauaji mengi ya Wanasayansi wa Iraq ni katika Operesheni za utawala huu ghasibu wa kizayuni.
- Amerika na nchi kadhaa za Magharibi hutetea vitendo hivi vya kigaidi vilivyo wazi kabisa, na ulimwengu wote unatazama tu!.
- Kulaaniwe vikali kupuuza kwa wadai wa Haki za Binadamu (na kufumbia macho) kwa mauaji ya Mashahidi wa takriban watoto 20,000 wa Kipalestina katika muda wa chini ya miaka miwili.
- Bila shaka watu wa mataifa mbalimbali ya dunia, yakiwemo ya Ulaya na Marekani, kwa kadiri wanavyojulishwa jinai hizo, wananafanya maandamano na mikusanyiko dhidi ya Wazayuni na Marekani, na iwapo taarifa kamili (ya jinai za wazayuni) itatolewa (ipassavyo), bila shaka mataifa hayo yatapanua maandamano yao.
- Kundi hili la wahalifu (la kizayuni linalofanya kazi ya uwakawala kwa niaba ya Wakoloni waliowahi kuikoloni Mashariki ya Kati), ni waovu na hatari na lazima liondolewe Palestina na eneo hili zima la kikanda, jambo ambalo litatokea kwa Mapenzi ya Mwenyezi Mungu (Insha Allah) na juhudi zaidi katika uwanja huu (katika kutimiza hilo) ni Wajibu wa Kidini, Kimaadili na wa Kibinadamu wa Wanadamu wote.
*Misimamo yetu iko wazi:
- Ishara juu ya uthabiti wa misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu eneo hili la kikanda
- Misimamo yetu ni thabiti na uadui (wa sasa) wa Amerika na utawala wa Kizayuni ni sawa na (uadui) wa huko nyuma.
* Kwa hakika watapokea kisasi cha pigo sawa na kali zaidi:
- Ikiwa uovu wowote utatokea kutoka nje, jambo ambalo bila shaka halipewi (ihtimali kubwa sana au) uwezekano wa kutokea, hakika watapokea kisasi cha pigo zito sana na kali zaidi.
- Iwapo adui, kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma, anafikiria kuunda fitna (na mitafaruku ya) ndani, Taifa litatoa jibu kali kwa wanaochochea fitina, kama ilivyokuwa kwa miaka iliyopita.
Your Comment