Kupitia mihadhara hii, waumini hupata fursa ya kujifunza misingi ya itikadi, maadili ya Kiislamu, na mwongozo wa maisha unaojengwa juu ya haki, uadilifu na kumcha Mwenyezi Mungu.
Uharibifu wa Jannat al-Baqii umeacha doa lisilofutika katika historia ya Uislamu. Makaburi haya hayakuwa tu sehemu ya kumbukumbu ya kihistoria, bali pia yalikuwa alama ya mapenzi na heshima kwa watu waliotumikia Uislamu kwa ikhlasi na kujitolea.
Leo hii, Waislamu kote duniani wanaendelea kuomba urejesheaji Heshima na Staha inayostahili kwa Makaburi haya matukufu.