Chuo cha Mabinti cha Hazrat Zainab (s.a) – Kigamboni - Dar-es-Salaam, ni Chuo bora kabisa nchini Tanzania kwa ajili ya Mabinti wa Kiislamu chenye usajili kamili kwa ajili ya kuendelea na harakati zake za utoaji wa maarifa katika:  1_Sayansi za Kiislamu (Islamic Sciences)  2_Na Sayansi za Kibinadamu (Humanities).

25 Oktoba 2025 - 15:00

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Waheshimiwa Wazazi: Uongozi wa Chuo cha Kidini cha Mabinti wa Kiislamu - Cha Hazrat Zainab (sa), kilichopo Kigamboni, Jijini Dar-es-Salaam – Tanzania unatumia fursa hii kukutangazieni juu ya uwepo wa fursa adhimu za Kielimu katika Chuo hiki kwa ajili ya Mustakbali Mwema wa mabinti zenu wapendwa.

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Bismillah Ar-Rahman Ar-Rahim

Kando na kupata Elimu ya Dini Tukufu ya Kiislamu, Mabinti zenu wapendwa wanaweza pia kupata elimu na ujuzi katika Kozi mbalimbali zenye umuhimu mkubwa katika mustakbali wao, ambazo zitawawezesha na kuwaongezea uwezo wa:

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

✅ Kupata ajira kwa haraka baada ya kuhitimu.

✅ Kujiajiri kwa kutumia ujuzi wa teknolojia.

✅ Kuendana na mabadiliko ya kidijitali duniani.

✅ Kuelekea kwenye taaluma zenye malipo mazuri.

Kwa Mantiki hiyo, Chuo cha Hazrat Zainab (sa) kinatoa Kozi zifuatazo kwa Mabinti wa Kiislamu:

1_Ushonaji na Ufundi Chereheni.

2_Kozi mbalimbali za Kompyuta.

4_Lugha ya Kiingereza.

5_Lugha ya Kiarabu.

6_Kozi ya Kilimo.

7_Masomo ya QT (Qualifying Test) – Kwa maana: Mafunzo ya Kidato cha Nne kwa wale waliokosa nafasi ya shule za kawaida.
8_Form Four Resitters – Masomo Mahsusi kwa ajili ya Kurudia Mtihani wa Kidato cha Nne.

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Kuhusu Chuo:

Chuo cha Mabinti cha Hazrat Zainab (s.a) – Kigamboni - Dar-es-Salaam, ni Chuo bora kabisa nchini Tanzania kwa ajili ya Mabinti wa Kiislamu chenye usajili kamili kwa ajili ya kuendelea na harakati zake za utoaji wa maarifa katika: 

1_Sayansi za Kiislamu (Islamic Sciences) 

2_Na Sayansi za Kibinadamu (Humanities).

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Kupitia kibali na usajili wake kamili, Uongozi wa Chuo hiki umeazimia na kukusudia kukusogezeeni fursa hizi muhimu kwa ajili ya Mabinti zenu Wapendwa, ambazo zitaanza rasmi katika mwaka mpya wa masomo wa 2026.

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Chuo kinapatikana: Kigamboni - Dar-es-Salaam 

Tanbihi:

1_Chuo cha Mabinti Kigamboni - Masomo yake yote yanaendeshwa kwa Lugha ya Kiingereza.

2_Mwanafunzi atakayepokelewa katika Chuo hiki ni yule aliyemaliza Form Four (Mwenye Cheti cha Form Four).

3_Mwanafunzi atafundishwa Lugha ya Kiingereza kwa muda wa mwaka mmoja ili kuimarishwa katika uzungumzaji na uelewa wa Lugha ya Kiingereza kwa kuzingatia kuwa Kiingereza ndio Lugha inayotumika katika Masomo yake yote katika Chuo hiki.

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

4_Mwanafunzi awe na Cheti cha Kuzaliwa au Namba ya NIDA.

5_Barua ya Mwenyekiti wa Mtaa.

6_Barua ya Uthibitisho ya Mzazi.

Tangazo la Nafasi za Masomo | Chuo cha Mabinti wa Kiislamu – Cha Hazrat Zainab (sa) Kigamboni Dar-es-Salaam, Tanzania + Picha

Wasiliana Nasi:

+255 745 993 522 | +255 745 002 259 | +255 781 119 113

Wahi kujisali - Nafasi ni Chache

Your Comment

You are replying to: .
captcha