Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wang Yi, Waziri wa Mambo ya Nje wa China, na Mohammad Ishaq Dar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, wamewasili mjini Kabul kwa ajili ya kushiriki kwenye mkutano wa pande tatu na Afghanistan.
Baada ya kuwasili, Waziri wa Mambo ya Nje wa China alipokelewa na Amir Khan Muttaqi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kaimu ya Afghanistan, na kufanya naye mazungumzo. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alipokelewa na Hanafi Wardak, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Taliban.
Inatarajiwa kuwa mawaziri hao wa mambo ya nje wa nchi tatu watakutana leo kwa mazungumzo ya pamoja juu ya ushirikiano wa kieneo hususan katika sekta za uchumi na biashara, miunganisho ya kikanda, pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi.
Aidha, kwa mujibu wa baadhi ya taarifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa China atakutana pia na baadhi ya viongozi wengine wa Taliban, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan akitarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na Amir Khan Muttaqi kuhusu masuala ya uhusiano wa nchi hizo mbili.
Your Comment