Spika wa Bunge la Iran ameandika kwenye ukurasa wake binafsi katika mitandao ya kijamii kuwa:“Kwa mwaliko maalumu wa Mheshimiwa Spika wa Bunge la Kitaifa la Pakistan, nimeelekea nchini humo.
Kuimarisha uhusiano wa pande mbili kati ya mataifa haya mawili ndugu - hususan katika nyanja za ushirikiano wa kiuchumi na kiusalama - kutakuwa ndiyo mhimili mkuu wa ziara hii.”
Waziri wa Mambo ya Nje wa China alipokelewa na Amir Khan Muttaqi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Kaimu ya Afghanistan, na kufanya naye mazungumzo. Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan alipokelewa na Hanafi Wardak, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Taliban.