Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– moto mkubwa ulizuka jioni ya Jumatatu, tarehe 13 Murdad (sawa na Agosti 4, 2025), katika misitu inayosimamiwa na Idara ya Kilimo ya Mkoa wa Bamiyan, hasa katika eneo la Shashpul.
Taarifa ya ofisi ya gavana ilisema kuwa moto huo ulidhibitiwa kikamilifu kwa juhudi za pamoja, na uharibifu uliotokea ulikuwa mdogo.
Hata hivyo, sambamba na tangazo hilo, vyanzo vya ndani katika mji wa Panjab viliripoti kuwa familia kadhaa za Wahazara na Waislamu wa Kishia walilazimishwa kuondoka katika kijiji cha Rashk kwa amri ya moja kwa moja kutoka kwa Mawlawi Sarhadi. Hatua hiyo imezua hofu kuhusu ongezeko la mashinikizo ya kimfumo dhidi ya jamii hizo nchini Afghanistan.
Wanaharakati wa kiraia pamoja na wakaazi wa eneo hilo wameutaja uhamishaji huo wa lazima kuwa ni uvunjaji wa wazi wa haki za binadamu, wakisema kuwa ni kielelezo cha ubaguzi wa kimfumo na mtazamo wa kiusalama wa Taliban dhidi ya jamii ya Wahazara na Waislamu wa Kishia.
Mmoja wa wakazi alilalamika: “Je, thamani ya miti michache ni kubwa kuliko maisha na hatima ya watu?”
Wakosoaji wanasema kuwa hatua za maonyesho za Taliban haziwezi kuficha ukweli wa ukandamizaji, unyang’anyi wa ardhi, uhamishaji wa lazima na dhulma dhidi ya makabila na madhehebu mbalimbali.
Jamii ya kimataifa na mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakionya mara kwa mara kuhusu hali ya hatari inayowakabili Wahazara na Waislamu wa Kishia katika mkoa wa Bamiyan na maeneo mengine ya Afghanistan – lakini hali hiyo inaonekana kuendelea bila mabadiliko yoyote.
Your Comment