13 Aprili 2025 - 16:44
Mubahatha  [Kudurusu kwa Pamoja] - Kwa wanafunzi na watafutaji elimu wote!

Ufahamu huwa na viwango tofauti tofauti, kwa malezi au asili. Wewe ambae ni Mwanafunzi katu usipuuze hichi kipengele cha majadiliano ya kielimu baada ya kupokea maarifa ya mada fulani kutoka kwa Mwalimu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Mubahatha  [Kudurusu kwa Pamoja] - Kwa wanafunzi na watafutaji elimu wote!
 
Ufahamu huwa na viwango tofauti tofauti, kwa malezi au asili.

Wewe ambae ni Mwanafunzi katu usipuuze hichi kipengele cha majadiliano ya kielimu baada ya kupokea maarifa ya mada fulani kutoka kwa Mwalimu.

Kunapokuwa na mjumuiko wa wanaojifunza, kwa hakika pale kuna matabaka ya ufahamu kadha na kadha, Na hali hiyo ni njema na nzuri mno!
Kuna ambao watafahamu kwa haraka a kuchakata maarifa waliyopata na kutengeneza maswali au kutatua mushkeli.

Na wapo ambao watafahamu kwa haraka ila hawana mifano au maarifa mengine ambayo yanaweza panua wigo wa ufahamu zaidi.

Pia kuna wale wataofahamu ila ni baada ya wao kurudia rudia mada husika waliyofundishwa.
 
Na kuna wale wanaotegemea kurejea tena kwa Wenzao wawafafanulie kile ambacho kilifundishwa ili na wao wakamate sawa sawa yale maarifa.
 
Makundi yote tajwa yananufaisha sana! Endapo kutakuwa na mjumuiko wa kujadili yale yalosomwa darasani.

Miongoni mwa faida za Discussion group [mijadala ya mijumuiko) ni:

1. Hukuza ufahamu zaidi

2. Hutoa ujasiri wa kueleza yale ulojifunza

3. Hurekebisha makosa au ufahamu usokusudiwa

4. Hujenga urafiki kwa wanaukumbi wa majadiliano

5. Hubakisha kile ulojufunza akilini kwa mda mrefuN.K

Ushauri:
   kama mtaani au kwenye nyumba moja au kwa jirani kuna wanafunzi wanaosoma darasa moja, basi wazazi na walezi wakutanisheni vijana wenu waweze kuunda ukumbi wa kudurusi kwa pamoja yale walojifunza darasani, alafu matunda yake mtanitupia moja walau dua.

Madrasat Bilal Moa Tanga Tanzania.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha