Mjadala
-
Kuendelea kwa Mjadala Mkali Kuhusu Mbio ya Hisani ya Msikiti wa East London; Wito Watolewa kwa Mapitio ya Sera ya Utenganisho wa Jinsia
Baada ya mashambulizi makubwa ya vyombo vya habari vya Uingereza dhidi ya mbio ya hisani iliyoandaliwa na Msikiti wa East London kwa sababu ya utenganishaji wa kijinsia, Tume ya Usawa na Haki za Kibinadamu ya Uingereza imeitangaza kwamba waandaaji wa tukio hilo wamekubali kupitia upya sera zake kabla ya awamu ijayo ya mashindano. Hata hivyo, msikiti huo umeeleza kwamba matukio kama hayo yapo kwa wingi katika maeneo mbalimbali ya Uingereza-ikiwemo mashindano maalumu ya wanawake na vipindi vya kuogelea vinavyoandaliwa katika vituo vya jamii ya Kiyahudi-lakini hakuna hata moja kati ya matukio hayo yaliyowahi kusababisha mjadala au msukosuko kama huu.
-
Utani wa Trump kwa Balozi wa Saudi Arabia Mjini Washington umeibua mjadala mkali
Video ya hotuba ya Rais wa Marekani katika kikao kilichofanyika Miami, ambapo alitumia mtindo wa utani akimtaja Balozi wa Saudi Arabia nchini Marekani, imesambaa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii na kuibua maoni na mjadala mkali miongoni mwa watumiaji.
-
Mzozo nchini Canada kuhusu uhuru wa kujieleza, kufuatia marufuku ya kuingia nchini kwa kundi la muziki linalounga mkono Ghaza
Utoaji wa muswada mpya na Waziri Mkuu wa Canada, unaolenga kukabiliana na uhalifu unaotokana na ueneaji wa chuki, pamoja na marufuku ya kuingia nchini kwa kundi la muziki la Kiayalandi lenye jina «NíACAB», umeanzisha mjadala mpana kuhusu mipaka ya uhuru wa kujieleza katika nchi hiyo.
-
Msimamo Mkali wa Hizbullah Dhidi ya Jaribio la Kuvunjwa kwa Silaha za Muqawama: Azimio Jipya la Serikali ya Nawaf Salam ni Tishio kwa Uhuru wa Lebanon
Chama cha Hizbullah kimetoa tamko kali kupinga uamuzi mpya wa serikali inayoongozwa na Nawaf Salam, ambao wanauona kama hatua ya hatari ya kudhoofisha muqawama (mapambano ya ukombozi) na kukabidhi usalama wa Lebanon kwa Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel. Katika taarifa hiyo, Hizbullah imesisitiza kuwa itakabiliana na uamuzi huu kwa msimamo thabiti kama hatua isiyokubalika kabisa, huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda silaha za kujihami na kuimarisha jeshi la taifa kwa ajili ya kutetea ardhi na uhuru wa Lebanon. Lebanon Bado Chini ya Vitisho vya Israel na Marekani
-
Katika kongamano la Kimataifa la "Sayansi, Dini, na Akili Bandia" lililofanyika Zagreb, Shahriyari:
Akili bandia si dhana bali ni mshirika kwa Binadamu katika kila dakika ya maisha yake
Katibu Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Kuleta Ukaribu wa Madhehebu ya Kiislamu alisema: Mjadala wa akili bandia ni mpana sana na unahusisha kila nyanja ya maisha ya binadamu, na kila mtu anapaswa kuuhusisha kulingana na wajibu wake mwenyewe.
-
Mubahatha [Kudurusu kwa Pamoja] - Kwa wanafunzi na watafutaji elimu wote!
Ufahamu huwa na viwango tofauti tofauti, kwa malezi au asili. Wewe ambae ni Mwanafunzi katu usipuuze hichi kipengele cha majadiliano ya kielimu baada ya kupokea maarifa ya mada fulani kutoka kwa Mwalimu.
-
Hatua Tano na Muhimu Kabla ya Kuingia Katika Mjadala au Kabla ya Kufanya Mjadala na Mtu yeyote | Bila hatua hizi huo sio Mjadala Bali ni Kupoteza Muda
Kabla hujafanya mjadala wowote na mtu yeyote, unapaswa kuzingatia nukta za kimjadala na muhimu ili uepuke mapema kupoteza muda wako kwa kuingia katika mjadala usiokuwa na matunda yoyote.