Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-Madrasat Al-Hadi Islamic Center nchini Malawi imeanza Mwanzo mpya wa kipindi kipya cha masomo kwa ari na hamasa kubwa. Siku ya kwanza ya masomo iliadhimishwa kwa hafla rasmi ya asubuhi, ikiwa ni sehemu ya kuashiria mwanzo wa safari nyingine ya kielimu na maendeleo.
Hafla hiyo ya asubuhi ilijawa na maneno ya hamasa, dua, na mawaidha kutoka kwa walimu na viongozi wa taasisi, wakihimiza wanafunzi kuwa na matumaini, kujituma, na kuwa na malengo makubwa katika safari yao ya elimu. Kwa pamoja, walisisitiza umuhimu wa nidhamu, juhudi, na mshikamano miongoni mwa wanafunzi na walimu ili kufanikisha mwaka wenye mafanikio.
Kauli mbiu ya mwanzo mpya ilikuwa: "Elimu ni ufunguo wa mafanikio - tukaze buti tangu mwanzo!"
Mazingira ya shule/taasisi yalipambwa vizuri kuonyesha hali ya ukaribisho na uzingatiaji wa mwanzo mzuri.
Wanafunzi wapya na wa zamani walipata fursa ya kujitambulisha, kushiriki katika dua ya pamoja, na kusikiliza hotuba zenye kuhimiza bidii, maadili na kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya mtu binafsi na jamii kwa ujumla.
Mwanzo huu umeleta ari mpya kwa walimu na wanafunzi, wote wakiahidi kushirikiana kwa karibu katika kuhakikisha elimu inatolewa kwa ubora na kwa ufanisi zaidi. Huu ni mwanzo wa safari mpya, yenye matumaini na mwanga wa mafanikio.
Your Comment