kielimu
-
Bi Mujtahida Saffati: Vyuo vya kidini vya wanawake vinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu wa wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu
Profesa mashuhuri wa vyuo vya kidini vya wanawake, katika hafla ya uzinduzi wa mwaka mpya wa masomo, alivitaja “ikhlasi na uchamungu (taqwa)”, “kuungana na uongozi wa Kiislamu (wilaya)”, na “kuzingatia haki za wengine” kuwa ni nguzo tatu muhimu za mafanikio kwa wanafunzi wa fani za dini. Akaeleza kwa msisitizo kuwa: Taasisi za kielimu za wanawake zinapaswa kuchukua uongozi wa kielimu kwa wanawake wa ulimwengu wa Kiislamu, na kutumia uwezo huo kwa ajili ya kusambaza maarifa ya Kiislamu katika ulimwengu mzima wa Kiislamu.
-
Malawi | Mwanzo Mpya wa Kipindi Kipya: Siku ya Kwanza, Marasimu ya Asubuhi Ikiashiria Matumaini na Mwelekeo wa Mafanikio katika Safari ya Kielimu
Kauli mbiu ya mwanzo mpya ilikuwa: "Elimu ni ufunguo wa mafanikio - tukaze buti tangu mwanzo!"
-
Ayatollah Rajabi:
Dhamira kuu ya Taasisi ya Imam Khomeini (rehmatullahi alayh) ni kuzalisha sayansi za binadamu za Kiislamu
Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi (Majlis Khobregan Rahbari) alisema kuwa Taasisi ya Imam Khomeini (rehmatullahi alayh) ina lengo kuu la kuzingatia nyanja kadhaa muhimu. Aliongeza kuwa taasisi hii inalenga sana masuala ya kielimu, maadili, pamoja na uelewa wa kijamii na kisiasa.
-
Kikao cha Kielimu na Utafiti kuhusu "Kumjua Mwenyezi Mungu (swt) Kujifunza Kuhusu"
Akinukuu Aya ya 108 ya Surah Yusuf, Sheikh Ghawth alisisitiza umuhimu wa kutumia akili, mazingatio na dalili za ulimwengu wa nje (Ulimwengu wa Dhahiri) katika kumuelewa Muumba.
-
Sheikh Abdul Ghani Khatibu | Maisha bila Malengo, ni Maisha yasokuwa na maana
Tukumbuke, maisha haya ni safari. Safari bila ramani hupotea. Weka malengo yako, yashike kwa mikono miwili, na muombe Allah akukadirie kheri na mafanikio ndani yake.