27 Oktoba 2025 - 21:12
Mkurugenzi wa Ofisi ya Jumuiya ya Kiislamu ya Ahlul-Bayt (a.s) nchini Lebanon akutana na Sheikh Ahmad Qablan

Mkutano huo uliandaliwa kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Bibi Zainab (a.s), ambapo Nakhai alitoa taarifa kuhusu maendeleo na utekelezaji wa programu mbalimbali za Jumuiya hiyo nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) -ABNA- Sheikh Ahmad Qablan, mmoja wa wanazuoni mashuhuri wa Lebanon anayejulikana kama “Mufti wa Jaafari”, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza mawasiliano ya kudumu na mapana kati ya Jumuiya ya AhlulBayt (a.s) na viongozi wa kidini kutoka dini na madhehebu mbalimbali.

Kauli hiyo aliitoa alipokutana na Hujjatul Islam Mohsen Nakhai, Mkurugenzi wa Ofisi ya Uwakilishi wa Jumuiya ya AhlulBayt (a.s) nchini Lebanon, ambaye alitembelea ofisi yake mjini Beirut kwa mazungumzo kuhusu masuala ya kielimu na kitamaduni nchini humo.

Mkutano huo uliandaliwa kwa mnasaba wa kuzaliwa kwa Bibi Zainab (a.s), ambapo Nakhai alitoa taarifa kuhusu maendeleo na utekelezaji wa programu mbalimbali za Jumuiya hiyo nchini Lebanon.

Sheikh Ahmad Qablan alibainisha kuwa, katika mazingira ya baada ya vita, kuimarisha uhusiano wa karibu na viongozi wa kidini ni jambo lenye baraka na linaweza kuchangia katika kuimarisha umoja wa kijamii na maelewano ya kidini.

Aidha, Sheikh Hassan Sharifeh, Imamu wa Msikiti wa As-Safaa mjini Beirut, aliambatana na Hujjatul Islam Nakhai katika ziara hiyo.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha