30 Machi 2025 - 23:52
Baadhi ya harakati za Kidini za Taasisi ya Kiislamu ya S.D.O - Bukoba, Tanzania

Kwa mtu yeyote, anayetaka thawabu na malipo mema toka kwa Allah (s.w.t), kupitia kusapoti na kusaidia Harakati hizi za Kidini za S.D.O Bukoba, Tanzania, basi anakaribishwa na mlango upo wazi.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA-; Taasisi ya Kiislamu ya S.D.O (Shiat Development Organization), Bukoba, Tanzania, inafanya kazi maridhawa za kusambaza Elimu na Maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s).

Baadhi ya harakati za Kidini za Taasisi ya Kiislamu ya S.D.O - Bukoba, Tanzania

Taasisi hii, inamiliki vituo Vitatu vya Kidini: 

Kituo cha Kwanza kipo Bukoba Mjini, ambacho kina Wanafunzi wa Day 68, Darasa la kina Mama Wanafunzi 17. 

Kituo cha pili, kipo Kemendo, katika Wilaya ya Bukoba,  Km 18 kutoka Manispaa ya Bukoba. Kituo hiki kina Darasa la kina Mama 33. Wanafunzi wa boarding Wanafunzi 20, na Wanafunzi wa Day 63. 

Kituo cha tatu, kipo Katobago, Km 89 kutoka Bukoba Mjini. Kituo hiki kina jumla ya Wanafunzi 52 wa Day, Wavulana kwa Wasichana, na Darasa la kina Mama 12.

Vituo hivi vinaendeshwa na kusimamiwa katika hali ngumu sana, lakini pasina kukata tamaa na kuzidi kupambana katika kuielimisha Jamii ili iweze kuyatambua Madhehebu ya Haki ya Ahlul-Bayt (a.s) na kufuata na kushikamana na Thaqalayni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na Itrah wa Mtume, Ahlulbayt Muhammad (s.a.w.w).

Kwa mtu yeyote, anayetaka thawabu na malipo mema toka kwa Allah (s.w.t), kupitia kusapoti na kusaidia Harakati hizi za Kidini za S.D.O Bukoba, Tanzania, basi anakaribishwa na mlango upo wazi.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha