21 Julai 2025 - 23:29
Hatima ya Watesi wa Ahlul-Bayt (a.s) | Waliomuua Imam Hussein (a.s) na Historia ya Kisasi na Kuangamizwa kwao

Wauaji wa Imam Hussein (as) walipata mmoja mmoja Hukumu za Kidunia kwa kumwaga Damu Takatifu ya Mjukuu wa Mtume Muhammad (saww) katika Ardhi ya Karbala

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Maelezo ya kihistoria yenye uzito kuhusu malipo ya hapa duniani kwa wauaji wa Imam Hussein (a.s) na wafuasi wake. 

Sheikh letu, Sheikh Hassan Busi, ametuandalia toleo zuri kuhusiana na hilo na ni kama ifuatavyo:

Malipo ya hapa duniani kwa wauaji wa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake – Sehemu ya 11:

Hatima ya Watesi wa Ahlul-Bayt (a.s) | Waliomuua Imam Hussein (a.s) na Historia ya Kisasi na Kuangamizwa kwao

15. Amru Bin bin Al-Hajjaji

Amru bin Hajjaji Az-Zubaidiy alikimbilia kijijini baada ya kushuhudia kuuawa kwa imam husayn (a.s). Wafuasi wa Mukhtar wakamkuta njiani akiwa amekufa kwa kiu. Wakakata kichwa chake na kukipeleka kwa Mukhtar.

16. Amru Bin Harith

Mukhtar (rahimahullah) alikusanya wafuasi wake nyumbani kwa ibrahim bin Malik Al-ashtar na kupanga kumuua amru bin hariyth, aliyekuwa liwali wa ubaidullah bin ziyad. Amru alikuwa na askari elfu nne, huku Mukhtar akiwa na mia mbili na Ibrahim akiwa na mia tatu.

Mukhtar alimwambia Ibrahim: "Nenda ewe Ibrahim, ikifika nusu ya mchana ingia kwa amru na umwambie kuwa watu wa basra wamemshinda ubaidullah bin ziyad, nami nimetoka kukuunga mkono. utakapompata, muue, kisha piga ngoma yake."

Ilivyofika mchana, Ibrahim na wenzake walipanda farasi hadi kasri ya Amru. Walipofika, Ibrahim akaingia akiwa na silaha. Mlinzi alimwuliza anataka nini, naye akajibu kwa hila ile ile ya msaada. amru alikuwa amelala ndani ya nyumba iliyofunikwa kwa katani, akiwa amevaa vazi la hariri lililochovywa dhahabu.

Alipofika barazani, ibrahim alikaribishwa. Walipokuwa wakizungumza, ibrahim aliona mkuki uliokuwa umefunikwa kwa kilemba cha hariri. alipohoji kuhusu mkuki, amru alisema: "huu ndio mkuki uliobeba kichwa cha husayn (a.s) toka kufa hadi Sham."

Ibrahim aliomba kuuona, na alipoupata akamchoma nao amru hadi mkuki ukatokea mgongoni. akakata shingo yake kwa upanga na kuwaangamiza walinzi wake. kisha alipiga ngoma, na majeshi ya amru walipowasili, ibrahim aliwaua wote waliotokeza. vichwa vyao vililetwa kwa mukhtar, naye akasujudu kwa kumshukuru allah.

17. Amru Bin Swabiyhi

Amru bin swabiyhi alikuwa akijivuna: "niliwachoma baadhi yao, niliwajeruhi, lakini sikumuua hata mmoja." Usiku, watu wa mukhtar walimkamata akiwa juu ya nyumba bila ya yeye kuhisi. upanga wake ulikuwa chini ya kichwa chake. walipomkamata, alisema: "Mwenyezi Mungu aujaalie upanga huu uwe mbaya." 

Alipelekwa kwa Mukhtar, akawekwa Kasri na asubuhi akafungwa pingu. Mukhtar akaagiza mkuki, akasema:

 "Mchomeni hadi afe." Akachomwa kwa mkuki hadi akafa.

18. Qais Bin Al-ash’ath

Qais bin al-ash’ath al-kindiy alipora chakula cha imam husayn (a.s) baada ya mashambulizi. mukhtar alimkamata, akamuua na kuchoma mwili wake moto.

19. Mwanaume kutoka Bani Kalbu

Imam husayn (a.s) aliposema: "ninywesheni maji", mwanaume mmoja kutoka bani kalbu akampiga mshale kwenye mdomo wa chini. imam akasema: "mwenyezi mungu asikate kiu yako." mtu huyo alipatwa na kiu isiyozimika hadi alipojitupa mtoni furati na kunywa kwa pupa hadi akafariki.

Rejea: Jihadi ya imamu husayn (a.s) na mapambano yake — sayyid muhammad al-hussayn shirazi, uk. 124–126.

Hatima ya Watesi wa Ahlul-Bayt (a.s) | Waliomuua Imam Hussein (a.s) na Historia ya Kisasi na Kuangamizwa kwao

Usikose sehemu ya kumi na mbili, tujifunze kuhusu malipo ya hapa duniani kwa wauaji wa imam husayn (a.s) na mashahidi wa karbala.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha