27 Machi 2025 - 02:37
Gwaride la Boti 3,000 za Kijeshi za Iran litafanyika kuwaunga Mkono Wananchi wa Palestina

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran limetangaza Gwaride la Boti za Kijeshi 3,000 na uhamasishaji wa Wananchi kwa ajili ya kuwaunga mkono Wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna-; Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetangaza kuwa: Katika mkesha wa Siku ya Quds Duniani na kwa ajili ya kuwaunga mkono Wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina, Gwaride la Boti 3,000 za Kijeshi na uhamasishaji wa Wananchi litafanyika siku ya Alkhamisi tarehe 27 Machi, 2025 katika Bandari zote za Ghuba ya Uajemi, Pwani ya Makran na Bahari ya Mazandaran.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha