23 Aprili 2025 - 19:25
Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) | Jua la Elimu na Uchaji Mungu Limezimwa

Shahada ya Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) haikuwa tu kumpoteza kiongozi wa kiroho, bali ilikuwa ni jaribio la kuangamiza nuru ya elimu na mwongozo wa Ahlul Bayt(a.s). Hata hivyo, athari ya mafundisho yake bado inaishi hadi leo kupitia Maktaba ya Ja’fariyya, ambayo ni msingi wa Madhehebu ya Shia Ithna ‘Ashari.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Tarehe 25 Shawwal – Ni kumbukumbu ya Tukio la Huzuni na Tafakari katika Umma wa Kiislamu. Katika historia ya Uislamu, tarehe 25 Shawwal hujulikana kama siku ya huzuni, ikikumbusha tukio la kusikitisha la shahada ya Imam wa sita wa Ahlul Bayt (a.s), Ja’far ibn Muhammad al-Sadiq (a.s). Imamu huyu alisimama katika zama ngumu za mabadiliko ya kisiasa kati ya utawala wa Bani Umayyah na Bani Abbas, na katika mazingira hayo alitumia fursa hiyo kuhuisha elimu na maarifa safi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) alifundisha maelfu ya wanafunzi na kuweka misingi ya elimu ya Kiislamu kwa upana, ikiwemo Elimu ya Fiqhi, Tafsiri ya Qur'an, Falsafa, Tiba, Fizikia na Kemia. Ujasiri wake katika kusema ukweli, msimamo wake wa haki, na bidii yake katika kufundisha Qur’an na Sunna sahihi, vilimfanya awe nuru ya maarifa katika giza la dhulma za watawala wa wakati huo.

Kumbukumbu ya Shahada ya Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) | Jua la Elimu na Uchaji Mungu Limezimwa

Lakini nuru hiyo haikupendwa na wafuasi wa dhulma. Khalifa wa Abbasiyya, Mansur al-Dawaniqi, akiwa na hofu juu ya ushawishi wa Imam katika jamii ya Kiislamu, aliamuru kuuawa kwake kwa njia ya sumu. Imam akafariki kifo cha Kishahidi akiwa na miaka 65, na akazikwa katika makaburi ya Baqi’, Madina.

Shahada ya Imam Ja’far al-Sadiq (a.s) haikuwa tu kumpoteza kiongozi wa kiroho, bali ilikuwa ni jaribio la kuangamiza nuru ya elimu na mwongozo wa Ahlul Bayt(a.s). Hata hivyo, athari ya mafundisho yake bado inaishi hadi leo kupitia Maktaba ya Ja’fariyya, ambayo ni msingi wa Madhehebu ya Shia Ithna ‘Ashari.

Katika kumbukumbu hii tukufu, tunakumbushwa kwamba elimu ni silaha ya mapambano dhidi ya ujahili, na kwamba viongozi wa haki daima watakumbwa na mateso kutoka kwa watawala wa batili. Ni juu yetu kuenzi njia ya Imam Sadiq (a.s) kwa kuendeleza elimu, kusimama na haki, na kulinda misingi ya dini kwa uaminifu na maarifa.

"السلام عليك يا جعفر بن محمد الصادق، يوم ولدت ويوم استشهدت ويوم تبعث حيا"

"Amani iwe juu yako, ewe Ja’far bin Muhammad al-Sadiq, siku ulipozaliwa, siku ulipouliwa kifo cha Kishahidi, na siku utakayofufuliwa ukiwa hai".

Makala hii fupi imeandaliwa na:

Sheikh Taqee Zachalia Othman.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha